Wanafunzi 42 Chuo cha LUHET washindwa kuendelea na masomo kwa kukosa ada

Na Amiri Kilagalila

Wanafunzi 42 wa kozi mbalimbali za afya waliokuwa wakisoma katika Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHET) wameshindwa kuendelea na masomo kwa changamoto ya kukosa ada.

Akizungumza katika mahafali ya 25 ya taasisi hiyo yaliyofanyika Julai 25, 2025 katika chuo hicho kilichopo Lugarawa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Buteye Dotto Buteye ambaye ni Mkuu wa LUHET amesema kuwa wanawapeleka sokoni wahitimu 320 lakini taasisi ilianza na wanafunzi 418, ambapo wanafunzi 84 walisimama masomo kwa changamoto mbalimbali huku kati yao wanafunzi 42 ikiwa ni changamoto ya ada.

“Kuna changamoto nyingi ambazo wanafunzi hawa wameweza kuzipitia lakini sababu ya kwanza ni ya kifedha na katika hao wanafunzi 84 ni wanafunzi 42 ambao taasisi ilipokea barua zao za kuahirisha masomo” amesema Buteye.

Buteye ameiomba Serikali kuongeza wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati ili kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi wanaosimama masomo yao kutokana na kushindwa kumudu gharama.

Baadhi ya wahitimu wa kozi mbalimbali kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHET), walioshiriki katika mahafali yaliyofanyika chuoni hapo Julai 25, 2025. Picha na Amiri Kilagalila.

Nae Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Eusebius Kyando ametoa rai kwa wanafunzi kuendelea kuitafuta elimu huku changamoto za kifedha zikiendelea kutatuliwa.

“Elimu tunaitafuta kwa hiyo ninawaasa msitoroke elimu,changamoto ya kifedha zinaeleweka na uongozi wa taasisi uendelee kutafuta ili kuona njia ya kuwasaidia wanafunzi wanaostahili kupata mikopo” amesema Askofu Kyando.

Baadhi ya wahitimu akiwemo Roziana Makana amesema kutokana mafunzo waliyopata wako tayari kwenda kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya afya na kutii viapo vyao huku pia wakijali utu na haki za wagonjwa.

Licha ya changamoto hiyo serikali imeshaanza kufanyia kazi ambapo baadhi ya kozi katika vyuo vya kati vimekuwa vikipata mikopo ikiwemo kozi ya maabara tiba, mionzi pamoja na kinywa na meno, ambapo katika Taasisi ya LUHET yenye kozi tano za afya ni kozi mbili pekee zilizopewa kipaumbele na kupokea mikopo.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW