COP 31: Viongozi kujadili mpango wa kuongeza matumizi ya umeme Duniani

Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kutoa hotuba zao leo Jumatano, Novemba 11, 2026 katika Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), unaoendelea jijini Antalya nchini Uturuki, huku mazungumzo yakilenga kuongeza matumizi ya umeme duniani na kuharakisha juhudi za kupunguza utegemezi wa nishati za mafuta ya kisukuku.

Wakati wajumbe kutoka takribani nchi 200 wakihudhuria mkutano huo, uzalishaji wa gesi chafuzi duniani bado haujaonyesha mwelekeo wa kushuka kwa kiwango kikubwa, ambapo hali hiyo inaendelea kuwa changamoto kutokana na dunia pia kushughulikia migogoro ya kivita, mfumuko wa bei na changamoto nyingine.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka huu imeonya kuwa dunia inaelekea kuvuka kiwango cha ongezeko la joto la nyuzi joto za selsiasi 1.5 kilichokubaliwa na mataifa chini ya Mkataba wa Paris, hatua inayozua wasiwasi kuhusu uwezo wa dunia kudhibiti athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ufaransa na Rais wa mkutano wa COP uliofanyika Paris mwaka 2015, Laurent Fabius amesema hotuba za viongozi zinaweza kutoa msukumo wa kisiasa katika mazungumzo yanayoendelea, akisisitiza kuwa jambo muhimu katika mkutano wa Antalya ni utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na mataifa badala ya kutoa matamko pekee.

Katika mkutano huo, Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen, Makamu wa Rais wa China Han Zheng na Rais wa Visiwa vya Marshall Hilda Heine ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhutubia leo, huku viongozi wengine wakitarajiwa kuhutubia hapo kesho, Novemba 12.

Wakati huohuo, Uturuki ambayo ni mwenyeji wa COP31 inapendekeza mataifa kuweka lengo la kuongeza kiwango cha umeme katika matumizi yote ya nishati duniani hadi asilimia 35 ifikapo mwaka 2035, kutoka kiwango cha sasa kinachozidi asilimia 20. Pendekezo hilo linakusudia kuongeza matumizi ya umeme katika sekta za usafiri, viwanda na majengo ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi.

Hata hivyo, pendekezo hilo limeibua maswali kwa kuwa halijaweka sharti kwamba umeme wote utakaoongezwa uzalishwe kupitia vyanzo vya nishati safi. Aidha, bado hakuna mpango mpana uliokubaliwa na mataifa kuhusu namna ya kuachana na matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi asilia, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres akiyataka mataifa kuweka ratiba zilizo wazi za kuachana na nishati hizo.

Kwa upande mwingine, Brazil ambayo iliandaa mkutano uliopita wa COP, imewasilisha mapendekezo ya hatua za kupunguza utegemezi wa nishati za mafuta ya kisukuku. Mpango huo unapendekeza mataifa kufanya tathmini na kupanga mifumo yao ya nishati ifikapo mwaka 2028, kabla ya kuanza kushirikiana kupunguza uzalishaji na upatikanaji wa nishati za mafuta ya kisukuku kuanzia mwaka 2031.

Marekani, ambayo ni miongoni mwa nchi zinazochangia kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa kihistoria wa gesi chafuzi, haishiriki mkutano huo kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya Rais Donald Trump kujiondoa katika ushirikiano wa kimataifa wa masuala ya tabianchi mwaka 2025.

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW