Mchengerwa: Tunataka tuwe huru kuzalisha dawa zetu wenyewe

Na Wizara ya Afya

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa uhamasishaji wa wawekezaji wa viwanda vya dawa nchini ni mpango wa Taifa ulioanzishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, shabaha ikiwa ni kuona Tanzania inajitosheleza kwa bidhaa hiyo lakini pia kuwa muuzaji kwa nchi zingine ifikapo mwaka 2030.

Waziri Mchengerwa amesema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kando ya Kongamano la Wazalishaji wa Dawa pamoja na Vifaa tiba leo Januari 19, 2026 katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.

“Huu ni mpango wa Taifa uliowekwa wazi ndani ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kuhakikisha nchi inakuwa na uhuru wa kuzalisha dawa zake yenyewe,” amesema Waziri Mchengerwa.

Waziri Mchengerwa amesema Taifa limejipanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2030, kiwango cha uzalishaji wa dawa kuongezeka kutoka asilimia 10 ya sasa hadi kufikia asilimia 65.

“Mpango huu ni mpango wa Taifa unaoongozwa na Rais, ili ifikapo 2030, baada ya Rais kustaafu, tuwe tumejitosheleza na tumepanda kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 65 ya uzalishaji wa dawa nchini,” amesema Waziri Mchengerwa.

“Hivi sasa tumepata wadau wa uwekezaji zaidi ya 40 kutoka mataifa mbalimbali, ikiwemo Ujerumani, Uingereza, Marekani na India, ambao watahakikisha changamoto zote zilizokumba sekta ya uzalishaji wa dawa zinatatuliwa kwa sababu wamejipanga vizuri” amefafanua Mchengerwa.

Aidha, Waziri Mchengerwa amesema kwa mipango hiyo ya Wizara ya Afya, Taifa litapiga hatua katika uzalishaji wa dawa ndani ya nchi, jambo litakalo okoa fedha za Serikali zinazotumika kuagiza dawa nje ya nchi na pia kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa wananchi.

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW