AZAKI: Wahanga wa Oktoba 29 walipwe fidia stahiki

Na Dominic Allen

Umoja wa Asasi za Kiraia Tanzania (AZAKI) umetoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwalipa fidia stahiki wahanga wote wa ghasia zilizotokea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 29, 2025.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 27, 2026 AZAKI wamesisitiza kuwa ulipaji wa fidia kwa waliofariki na waliojeruhiwa unapaswa kuzingatia sheria na mikataba ya kimataifa ya kufidia wahanga.

Hata hivyo, wamepinga pendekezo la Tume ya kuchunguza matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, iliyopendekeza serikali kuweka utaratibu wa kuhakikisha majeruhi waliopata ulemavu kutokana na ghasia hizo wanapata huduma za matibabu bure, ikiwa ni pamoja na vifaa saidizi na viungo bandia (prostheses), ambapo wametafsiri kuwa hiyo ni kejeli kwa wahanga, ndugu na jamaa.

Wakitilia mkazo suala la uwajibikaji, AZAKI wametaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika na mauaji na matumizi ya nguvu kupita kiasi, kama ilivyobainishwa katika taarifa ya Tume.

Kuhusu kuundwa kwa Tume ya maridhiano, AZAKI wameshauri mchakato huo unapaswa kuendana na utaratibu wa viwango vya kimataifa na weledi wa kutanzua migogoro, na kisimamiwa na watu waadilifu, ukihusisha makundi yote muhimu ya kijamii na kisiasa.

AZAKI pia wamesisitiza kuwa wafungwa wote wa kisiasa wanaoendelea kushikiliwa gerezani kuhusiana na matukio ya Oktoba 29, 2025 waachiliwe bila masharti yoyote, akiwemo Mwenyekti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, ambaye hadi sasa anakabiliwa na kesi ya uchochezi na uhaini.

Msimamo na wito huo wa Umoja wa Asasi za Kiraia Tanzania (AZAKI) umefuatia baada ya Tume ya kuchunguza matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu jijini Dar es Salaam Aprili 23, 2026.

Picha: BBC

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW