Na Dominic Allen
Wataalamu kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC) pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu leo Mei 28, 2025 wameendelea na ziara maalum Zanzibar ya mafunzo yanayohusu uendeshaji wa vituo vya matibabu kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP).
Katika ziara hiyo ya siku tano iliyoanza Mei 26, 2025 ambapo inatarajiwa kumalizika Mei 30, wataalamu kutoka PPPC pamoja na wahadhiri hao wakiongozwa na Afisa Miradi Kutoa Idara ya Usimamizi wa Miradi wa PPPC, Bw. Dakawa Msoleni, wamepata fursa ya kutembelea Idara ya Ubia Zanzibar na kupokelewa Kamishna wa Idara ya Ubia, Bw. Emmanuel Mashimba ambaye amesema kuwa uamuzi wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kusukuma ajenda za PPP kumechochea uboreshaji wa Sekta Binafsi kwenye uchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Wizara ya Afya Zanzibar, Dr. Hussein Marijani amesema Ubia kwenye Sekta ya Afya umeleta mabadiliko makubwa, ambapo ameeleza kuwa changamoto kadhaa ambazo zimesalia zinaendelea kushughulikiwa.


Ziara hii muhimu ambayo imelenga kuongeza maarifa kwa wataalamu wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC) pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu imefuatia baada ya kituo cha PPPC kuendesha zoezi la mafunzo na uibuaji miradi kwenye halmashauri zote nchini Tanzania.
Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway


