Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwepo Makamu Mwenyekiti bara Tundu Lissu , Katibu Mkuu John Myika, Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi, viongozi wa BAVICHA na vijana wengine waliokuwa wanaenda Mbeya katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe tayari amelaani tukio hili huku akitaka jeshi la polisi kuwaachia viongozi na vijana wa CHADEMA bila masharti yoyote.
Haya yanatokea ikiwa maadhimisho ya siku ya vijana hapa Tanzania yameadhimishwa na vijana kutoka vyama vingine vya CCM na ACT Wazalendo kwa nyakati tofauti.
Hadi sasa taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi iliyotolewa jana ni kuwa wamepiga marufuku maadhimisho ya siku ya vijana duniani yaliyopangwa na CHADEMA kufanyika jijini Mbeya kwa madai kuwa yatahamasisha vurugu. Hadi wakati huu hakuna idadi kamili ya vijana wa CHADEMA wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi.
Kabla ya Katibu Mkuu wa CHADEMA John Myika kukamatwa, alimtaka Rais kuzuia kamata kamata inayofanywa na jeshi la polisi kwa sababu inaenda kinyume na 4R ambazo Rais Samia alizinadi mara baada ya kuingia madarakani.
Tangu mwaka 1999 maadhimisho ya siku ya vijana duniani hufanyika tarehe 12 ya mwezi Agosti kila mwaka yakibeba ajenda mbalimbali za vijana.




