Changamoto ya malisho ‘Vijana wa Loliondo, Sale wamuomba Dkt. Bashiru kuingilia kati’

Na Dominic Allen

Tatizo la ukosefu wa maeneo ya kutosha kwa ajili ya malisho kwa wakazi wa Tarafa ya Sale na Lolindo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha limeendelea kuwa pigo kwao, ambapo baadhi wamekuwa wakilazimika kulisha hifadhini au pembezoni mwa hifadhi ili kunusuru mifugo yao, jambo ambalo linalopelekea kukamatwa kwa mifugo na kupigwa faini kuanzia kiasi cha Shilingi za Kitanzania Laki moja.

Kufuatia changamoto hiyo ya kukosekana kwa maeneo ya malisho, vijana wa jamii ya wamasai kutoka Tarafa ya Sale na Loliondo wameandika barua kwenda kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuingilia kati suala hilo kwani ni mwiba kwao, ikizingatiwa kuwa shughuli za ufugaji ndiyo chanzo kikubwa cha mapato katika maisha yao ya kila siku.

“Kwa heshima kubwa, naomba kuwasilisha kwako hoja hii ya kisera kwa lengo la kuomba uratibu wa serikali kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na wadau wengine wahusika, ili kushughulikia changamoto kubwa inayowakabili wafugaji nchini hasa wilaya ya Ngorongoro, hususan katika Tarafa za Loliondo na Sale, kutokana na kiangazi kikubwa cha mwaka huu pamoja na umegaji wa ardhi ya malisho kwa ajili ya Pori la Akiba la Pololeti,” imeleeza barua hiyo.

Vijana kutoka Tarafa ya Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha katika picha ya pamoja wakati wakizungumzia tatizo la ukosefu wa maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Katika barua hiyo, vijana hao wamesema hadi sasa wakazi kutoka zaidi ya vijiji 14 katika Kata 8 za Tarafa ya Sale na Loliondo, wamekumbana na rungu la kukamatiwa mifugo yao, ambapo wameeleza kuwa faini ambazo zimekuwa zikipigwa na mamlaka husika zimekuwa ni mzigo kwao.

“Kumekuwepo na ukamataji mkubwa wa mifugo kwenye maneo yaliyohifadhiwa, hasa pori la Akiba la Pololeti (PGR), hali ambayo imeathiri zaidi ya vijiji 14 kwenye kata 8 vilivyopo katika tarafa tajwa. Aidha, faini ya shilingi 100,000 kwa kila ng’ombe anayekamatwa imeendelea kuwa mzigo mkubwa kwa wafugaji,” wamesema vijana hao.

Wakizungumzia suala la mabadiliko ya tabianchi na umegaji wa ardhi ya malisho, wamesema jambo hilo limechochea njaa kwa mifugo kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa maeneo ya malisho na vyanzo vya maji.

“Hali hii inaathiri utekelezajiwa Malengo ya Sera ya Taifa ya Nyanda za Malisho, inayolenga matumizi endelevu ya rasilimali za malisho, kuzuia uharibifu wa mazingira, na kulinda maisha ya wafugaji dhidi ya majanga ya asili ikiwemo ukame,” imeeleza barua hiyo.

Hali ya kiangazi pamoja na ukosefu wa maeneo ya malisho umesababisha kudhoofu na kufa kwa mifugo, jambo ambalo limeathiri uchumi wa waa wakazi hawa ambao hutegemea zaidi ufugaji kama chanzo chao kikuu cha mapato.

Kutokana hali ya kiangazi na ukosefu huo wa maeneo ya malisho, vijana hao kutoka Tarafa ya Sale na Loliondo wameiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa ruhusa maalum kwa muda, ili walishe mifugo yao katika baadhi ya maeneo ya hifadhi.

“Bila kuathiri wala kuingilia mwenendo wa kesi zilizopo mahakamani Pamoja na majibu ya Tume ya Rais kuhusu maeneo husika, tunaomba serikali izingatie uwezekano wa kutoa ruhusa ya muda, ya kisera naya kiserikali, kwa wafugaji kulisha mifugo yao kwenye baadhi ya maeneo ya hifadhi wakati wa vipindi maalum ya kiangazi kikubwa au wakati wa vipindi vigumu ili kunusuru maisha ya mifugo na watu kwa ujumla.”

Hata hivyo, vijana hao wanaona kuwa ni vyema serikali kutazama upya suala hilo, kwani kitendo cha mifugo yao kufa kutokana na kukosa malisho, kuhatarisha moja kwa moja uchumi wa jamii nzima.

“Kukubali mifugo kufa kwa wingi kutokana na kukosa malisho, ilihali kuna maeneo yenye nyasi ambayo yanaweza kutumika kwa udhibiti maalum bila kuathiri uhifadhi, ni kuhatarisha moja kwa moja Uchumi wa jamii nzima, kuongeza umasikini, na kudhoofisha juhudi za kitaifa za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,” wameeleza vijana hao.

Wakiwa na imani na ofisi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wameiomba kuratibu mazungumzo ya kisera na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na mamlaka husika, ili lipatikane suluhisho la muda na la kudumu ambalo litasaidia katika kukabiliana na athari za kiangazi kikubwa kwa wafugaji bila kuathiri uhifadhi wa maliasili za Taifa.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW