Dkt. Catherine, Ubunge Viti Maalum Wazazi “Anatosha”

Na Mwandishi wetu

Mnamo Juni 29, 2025 Dkt. Catherine Joachim ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Afya na Mazingira Umoja wa Wazazi Taifa, Jumuiya ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum Wazazi Tanzania Bara. Hatimaye baada ya kufanyika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wa Chama Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kamati Kuu imemuamini Dkt. Catherine na kulirejesha  jina lake kwa upande wa Tanzania Bara.

Dkt. Catherine Joachim ni nani?

Dkt. Catherine Joachim ni daktari wa binadamu, mbobezi katika uimarishaji wa huduma za afya na  mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika masuala ya uongozi nchini, kisera na utekelezaji ambao umekuwa na matokeo chanya kwa jamii.

Akitumia taaluma yake na uzoefu ipasavyo, Dkt. Catherine kwa nyakati tofauti tofauti amefanya kazi katika Sekta ya Umma na Binafsi, akichangia katika utekelezaji wa Sera ya Afya, lishe na uratibu kwa kisekta nchini.

Kada huyu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amekuwa akijitoa kwa chama na jumuiya zake zote, wengi wanamuona kuwa ni tunu na mfano wa kuigwa, Jumuiya ya Wazazi inajivunia uwepo wake kutokana na utendaji kazi na kujitoa kwake.

Dkt. Catherine Joachim mgombea wa nafasi ya Ubunge Viti Maalum Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Wazazi.

Baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuonesha imani kwake na kulirejesha jina lake kwa upande wa Tanzania Bara, Dkt. Catherine ameweka vipaumbele ambavyo atahakikisha anavitekeleza endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum Wazazi Tanzania Bara;

Dkt. Catherine amesema kuwa endapo atapata ridhaa na kuchaguliwa katika nafasi hiyo ya Ubunge wa Viti Maalum Wazazi Tanzania Bara, kupitia sauti ya wazazi katika ngazi zote anachangia kwa vitendo utekelezaji na ufuatiliaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025 – 2030.

Pia atahakikisha anashiriki ipasavyo katika kutekeleza na kufuatilia mikakati ya Jumuiya ya Wazazi, ili kuimarisha jamiii kuanzia ngazi ya familia, kwani ndiyo msingi wa Taifa, huku akiwaunganisha wazazi na fursa za kiuchumi , uwekezaji na ujasiriamali lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kujitegemea.

Mbali ya hayo yote, kuchaguliwa kwa Dkt. Catherine kutatoa nafasi ya kumwezesha kuwakilisha sauti ya wazazi katika mabaraza na ngazi za maamuzi ya kitaifa.

Duru mbalimbali za kisasa nchini zinamtaja kama kiongozi mwenye maono, mpenda watu asiye na makundi, mpatanishi na si mchonganishi, mwenye uwezo wa kusimama na kutetea maslahi ya Jumuiya ya Wazazi na watu wake. Mpambanaji katika masuala ya elimu ,uchumi na maendeleo, mwenye uthubutu wa kufanya jambo kwa ajili ya wengine.

Wadadisi wa mambo wamebainisha kuwa Dkt. Catherine ana nafasi kubwa katika uchaguzi huu, akiwa na ushawishi na mwenye mvuto, hivyo kumpoteza ni kupoteza rasilimali muhimu katika Jumuiya ya Wazazi. Na wanakubaliana na hilo wamesema Dkt. Catherine Joachim anatosha na wanatamba nae.


Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW