Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo Novemba 24, 2026, imetangaza timu ya taifa ya Senegal kuwa mabingwa wa AFCON baada ya pingamizi lililowasilishwa na Shirikisho la Soka la Morocco kuhusu ubingwa huo.

CAS imethibitisha matokeo yaliyopatikana uwanjani na kuamua kuwa Senegal ndiyo washindi, ikiwa ni takribani miezi 10 tangu fainali hiyo ilipochezwa.

Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), iliyochezwa Januari 18, 2026, nchini Morocco, ilizua mvutano baada ya Senegal kuifunga Morocco bao 1-0 kupitia muda wa ziada.

Hata hivyo, mchezo huo uliingia kwenye mgogoro baada ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani kwa muda kupinga uamuzi wa mwamuzi wa kutoa penalti kwa Morocco katika dakika za mwisho za mchezo.

Baadaye, Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ilibatilisha ushindi wa Senegal na kuitangaza Morocco kuwa mshindi kwa mabao 3-0.

Senegal ilipinga uamuzi huo na kuwasilisha rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), ambayo imetengua uamuzi wa CAF, hatua inayomaliza mvutano huo.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW