Tanzania na Malawi zasaini Hati ya Makubaliano katika Afya na Mkataba wa kuhamisha wafungwa

Na Dominic Allen

Tanzania na Malawi zimesaini hati ya makubaliano katika sekta ya afya na mkataba wa kuhamisha wafungwa , ikiwa ni hatua ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa haya mawili jirani.

Makubaliano hayo yamesainiwa jana Februari 26, 2025 wakati wa Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo aliyeongoza ujumbe wa Tanzania alisaini makubaliano hayo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Nancy Tembo ambaye pia alisaini makubaliano hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Nancy Tembo wakisaini Hati ya Makubaliano hayo.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kombo amesema kusainiwa kwa makubaliano haya ni moja ya mafanikio ya mkutano huo na ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi.

Waziri Kombo pia amezihimiza taasisi na sekta husika kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa kwa tija na ufanisi ili kuleta manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Nancy Tembo amepongeza hatua hiyo muhimu na kubainisha kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo ni chachu ya mabadiliko katika sekta za afya na haki za wafungwa.

Waziri Tembo ameongeza kuwa ushirikiano huo utaimarisha huduma za afya na kusaidia katika kusimamia haki za wafungwa walioko katika magereza ya mataifa hayo.

Mbali na kusainiwa kwa makubaliano hayo, mkutano huo pia umejadili maeneo mengine ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi, yakiwemo biashara, elimu, miundombinu, nishati, na usalama wa mipaka.

Viongozi wa pande zote mbili wameahidi kuhakikisha kuwa uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa hayo unaendelezwa kwa manufaa ya wananchi wao.

Pia, wamekubaliana kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo unapaswa kufanyika kwa wakati ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa na kuongeza ushirikiano wa pande mbili kwa kiwango cha juu zaidi.

Mkutano huo wa JPCC ulitanguliwa na kikao cha Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania na Malawi uliofanyika tarehe 25 Februari 2025.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW