Katoni 1,162 za mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku zakamatwa jijini Mwanza

Na Dominic Allen

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limesema kuwa katika operesheni ambazo limekuwa likizifanya katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Januari 20 hadi Februari 20, 2025, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 21 wa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya kukutwa na mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku na serikali ya Tanzania kwa mujibu Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki za Mwaka 2019.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa siku ya jana Februari 20, 2025 amesema kuwa katoni 1,162 za mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku zimekamatwa mkoani Mwanza pamoja na mtumbwi mmoja ambao ulikuwa ukitumiwa kusafirishia mifuko hiyo na kuiingiza katika mialo iliyopo katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa RPC Mutafungwa, mnamo Februari 12, 2025 katika mtaa wa Nyangulugulu, Ilemela jijini Mwanza, Jeshi la Polisi liliwakamata Stanslaus Chacha Weria (22) mkazi Kata ya Guta wilayani Bunda mkoani Mara ambaye ni mfanyabiashara, pamoja na Byabato Prudensi Gideon (34) mkazi wa wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, baada ya kuwakuta na katoni 1162 za mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku.

Katika operesheni hiyo Jeshi la Polisi lilifanikiwa pia kuukamata mtumbwi wa MV Kabula 1 wenye namba za usajili TMZ 01245 ambao ulikuwa unatumika kusafirisha mifuko hiyo ndani ya Ziwa Victoria.

Mifuko ya plastiki ikionekna katika soko la Kirumba Jijini Mwanza ambapo hutumika kufungia bidhaa mbalimbali. Picha na Yohani Gwangway

RPC Mutafungwa amesema kuwa upelelezi bado unaendelea ili kudhibiti mtandao mzima unaojihusisha na biashara hiyo haramu ili wahisika wote wachukuliwe hatua za kisheria, ambapo ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linashirikiana kwa ukaribu na taasisi nyingine za serikali ikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kukomesha uhalifu huo wa unaohusisha mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku nchini.

Kukamatwa kwa mifuko hiyo ya plastiki jijini Mwanza kunafuatia baada ya uchunguzi wa Land Dwellers ambao ulibaini kuwa bado kuna usambazaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza licha ya katazo la serikali.

Katika uchunguzi huo, Land Dwellers ilitoa rai kuwa ili kuondokana na tatizo la matumizi ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku hapa nchini, Taasisi zinazohusika na mazingira kama Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Shirika la Viwango Tanzania  (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji Tanzania pamoja na taasisi nyingine zinapaswa kutengeneza mtandao wa pamoja ambao utaboresha zaidi ushirikiano wao katika utendaji kazi wa pamoja ili kuhakikisha usimamizi wa mazingira unapewa kipaumbele na unafikia lengo lililowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na pamoja na kanuni zake.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW