Dkt. Gwajima: Maafisa Maendeleo ya Jamii kuweni chachu ya mabadiliko

Na Dominic Allen

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwaelimisha wananchi kuhusu fursa mbalimbali zinazoweza kuboresha maisha yao.

Dkt. Gwajima ametoa wito huo wakati wa kufunga Kongamano la Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani Iringa hapo jana ambapo amesema kuwa kazi ya serikali sio kutunga sera pekee bali pia kuibua fursa na kuwawezesha wananchi.

“Dhamira ya serikali ni kuhakikisha jamii zinapiga hatua kimaendeleo. Kazi yenu haipaswi kuwa kutekeleza sera pekee, bali kubuni na kusaka fursa zitakazosaidia wananchi kushinda changamoto zao za kiuchumi na kijamii” alisema Dkt. Gwajima.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano la Maafisa Maendeleo ya Jamii lililofanyika mkoani Iringa.

Vilevile Dkt. Gwajima amekumbusha juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo itaadhimishwa Machi 8, 2025, huku akiwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa siku hiyo.

“Ninawaomba mshiriki kikamilifu katika shughuli zote za maadhimisho zitakazofanyika katika maeneo yenu, ikiwemo makongamano ya Kanda mbalimbali. Pia, shirikianeni na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ili waweze kushiriki ipasavyo na kufanikisha malengo yetu ya kuwawezesha wanawake” ameongeza Dkt. Gwajima.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Doris Kalasa amesema kuwa kongamano hilo limekuwa jukwaa muhimu la kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii ili kuongeza ufanisi wao katika kutekeleza majukumu yao.

“Nina imani kwamba kongamano hili limewapatia maarifa mapya na mbinu bora za kusimamia maendeleo ya jamii kwa weledi na uaminifu. Nendeni mkayatumie kwa vitendo ili kuleta mabadiliko chanya” alisema Kalasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James amemshukuru Waziri Dkt. Dorothy Gwajima kwa jitihada zake katika kukuza ustawi wa jamii na kupambana na ukatili wa kijinsia, akisisitiza kuwa amekuwa chachu ya mabadiliko kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii.

“Mheshimiwa Waziri, tunatambua na kuthamini mchango wako mkubwa katika kuhakikisha Maafisa Maendeleo ya Jamii wanapata mwongozo sahihi wa kuboresha maisha ya wananchi” alisema Kheri James.

Kheri James amemhakikishia Dkt. Gwajima kuwa mkoa wa Iringa utaendelea kuyatumia mafunzo hayo kwa vitendo ili kuleta maendeleo ya kweli katika jamii.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW