Serikali kuimarisha Kliniki Maalum kukabiliana na Selimundu

Na Wizara ya Afya

Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea amebainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko mbioni kuanzisha na kuimarisha kliniki maalum za kukabiliana na ugonjwa wa Selimundu kuanzia ngazi za chini.

Dkt. Nyembea amesema hayo Februari 20, 2024, wilayani Uyui, Tabora wakati wa zoezi la usimamizi shirikishi ambalo linaendelea mkoani humo na wataalam kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Timu ya Usimamizi wa Afya Mkoa.

Dkt. Nyembea amesema tayari serikali imeshaanza kugawa miongozo ya huduma za Selimundu kwa watoa huduma katika baadhi ya halmashauri nchini, lengo likiwa ni kuboresha hali ya utoaji wa huduma za Selimundu hasa katika zahanati na vituo vya afya vya pembezoni.

“Kwenye vituo vya afya ngazi ya chini watumishi watafundishwa namna ya kuwahudumia watoto na wote wenye uhitaji wa kupatiwa huduma za Selimundu lakini pia dawa za kuongeza damu na kutuliza maumivu zitatolewa ili wasipate madhira yanayotokana na ugonjwa wa Selimundu” amesema Dkt. Nyembea.

Dkt. Nyembea ameongeza kuwa mkoa wa Tabora ni miongoni mwa maeneo yenye wagonjwa wa Selimundu na tayari kwenye hospitali na vituo kuna wagonjwa wanaohudhuria kliniki na kupatiwa huduma, jambo linaloisukuma zaidi serikali kuanzisha kliniki maalum kwa ajili ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Daktari wa Magonjwa Yasiyoambukiza Dkt. Joseph Werema ambaye pia ni mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza wilaya ya Uyui mkoani Tabora amesema wilaya hiyo imewatambua wagonjwa 756 wa selimundu kwa mwaka 2024 ambapo kati yao 398 wana umri chini ya miaka mitano (5) na 358 wanaumri zaidi ya miaka mitano (5).

Wilaya ya Uyui imefikia hatua hiyo kupitia huduma za kliniki ya Selimundu ambazo zinatolewa katika hospitali ya wilayani hapo na vituo vitatu vya afya vya Ilolangulu, Upuge na Igalula.

“Mikakati iliyofanikisha kliniki za Selimundu ni kutokana na watoa huduma kujengewa uwezo, kuhakikisha dawa na vitendanishi vinapatikana muda wote, kufanya usimamizi shirikishi katika vituo vyenye kliniki za Selimundu, kufanya uhamasishaji katika jamii juu ya utambuzi na upimaji wa Selimundu ambapo pia tumekuwa tukishirikiana na wadau (World Vision Tanzania) katika kuwezesha huduma mkoba za Selimundu” alisema Dkt. Werema.

Mhariri: Dominic Allen.

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW