Watoa huduma za optometria waaswa kuzingatia sheria na kanuni ili kuilinda jamii

Na Atley Kuni, (WAF)

Msajili wa Baraza la Optometria, Sebastiano Millanzi amewataka wamiliki wa vituo vinavyotoa huduma za optometria vikiwemo kliniki, maabara , wasambazaji wa bidhaa za miwani tiba, fremu za miwani na lenzi tiba kutoa huduma bora kwa jamii kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili kuilinda jamii.

Millanzi ametoa rai hiyo Februari 19, 2025 wakati wa zoezi la usimamizi shirikishi kwa kuwakumbusha wamiliki wote wajibu wanaotakiwa kuutekeleza kabla ya kuanza kutoa huduma hizo.

“Ili kulinda afya ya macho ya jamii yetu ni marufuku kituo chochote kutoa huduma za optometria bila ya kuwa na mtaalam wa Optometria aliyesajiliwa na Baraza la Optometria na aliye na leseni hai, kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na atakayebainika hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, ” amesema Millanzi.

Millanzi ambaye ameongoza jopo la wataalam kutoka Wizara ya Afya amefanya zoezi hilo katika vituo mbalimbali vilivyopo mkoani Mwanza ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, St. Clara, Hospitali ya Kamanga na Kalisa Optometry Centre.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Millanzi amewakumbusha wamiliki wa vituo vinavyotoa huduma ya optometria kuhakikisha hawawatumii watu wasio na taaluma hiyo yaani (vishoka) kutoa huduma hizo.

“Baraza lipo kwa ajili ya kuwasimamia wataalam wa optometria ikiwemo kuwasajili, mara baada ya kukidhi vigezo vikiwemo kuhitimu mafunzo ya optometria kwa ngazi ya Stashahada au zaidi katika vyuo vilivyo na sifa na kufaulu, hivyo tukikuta watu wanatekeleza majukumu hayo bila ya kuwa na utaalam watachukuliwa hatua ikiwemo kufunga kituo husika” amesisitiza Millanzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamiliki wa vituo wamekiri kupokea ushauri na kuahidi kuzifanyia kazi kasoro zilizopo.

James Apollo ambaye ni Katibu wa Afya katika Hospitali ya St. Clara iliyopo Nyahingi amekiri uwepo wa Mapungufu na kuahidi kuchukua hatua za dharura ili kutatua tatizo linalowakabili ikiwepo kuajiri mtaalam aliyefuzu mafunzo ya Optometria.

Mwandishi: Atley Kuni, (WAF)

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW