Bilionea maarufu duniani ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Adani Group ya India, Gautam Adani na wengine saba wamefunguliwa mashtaka mjini New York, Marekani kwa tuhuma kutoa rushwa ya dola za Kimarekani milioni 265 kwa maafisa wa serikali ya India ili kupata mikataba ambayo ingeleta faida ya dola za Kimarekani bilioni 2 katika kipindi cha miaka 20.
Tayari Mahakama mjini New York imetoa hati za kukamatwa kwa Gautam Adani na mpwa wake Sagar Adani na waendesha mashtaka wanapanga kukabidhi hati hizo kwa vyombo vya sheria vya kigeni.


