Watu 13 wamepoteza maisha, 84 waokolewa Kariakoo, Dar es Salaam

Watu 13 wamepoteza maisha na wengine 84 wameokolewa kufuatia kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Dar es Salaam Novemba 16, 2024.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na wananchi kwa njia ya vyombo vya habari akiwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Samia amesema kuwa serikali itabeba gharama za matibabu kwa majeruhi na mazishi kwa waliopoteza maisha kufuatia kuanguka kwa ghorofa Kariakoo, Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Zainab Katimba (kulia) akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu), William Lukuvi (katikati) pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu (kushoto), walifika katika eneo la tukio Kariakoo, Dar es Salaam Novemba 17, 2024.

Hata hivyo Rais Samia amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongozana na wakaguzi wa majengo kukagua majengo eneo lote la Kariakoo ili kupata taarifa kamili ya majengo hayo, huku akilitaka Jeshi la Polisi Tanzania kupata taarifa kamili ya jengo lililoporomoka.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW