NEMC: Zaidi ya tani 150 ya vifungashio vya plastiki visivyokidhi viwango vimekamatwa

Na Dominic Allen

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware Semesi amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2024/25 zaidi ya tani 150 za vifungashio vya plastiki visivyokidhi viwango vilikamatwa maeneo mbalimbali nchini.

Dkt. Semesi amebainisha hayo leo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, wakati akielezea utendaji kazi wa NEMC katika kipindi cha miaka minne.

Ameongeza kuwa vifungashio hivyo ambavyo havikukidhi viwango vilitaifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa sheria.

Katika udhibiti wa vifungashio vya plastiki, Dkt. Semesi ametoa wito kuwa suala la udhibiti wa vifungashio vya plastiki ni jukumu la kila mtu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.

“Hata hivyo suala la udhibiti wa vifungashio vya plastiki ni letu sote kuanzia ngazi za familia hadi taifa, hivyo hatuna budi kushirikiana kwa ajili ya kuleta matokeo chanya” amesema Dkt. Semesi.

Dkt. Semesi atahadharisha kuwa taka za plastiki zina madhara makubwa kwa binadamu na mazingira kwa ujumla, hivyo kila mmoja anatakiwa kusimama kwa nafasi yake kuhakikisha mifuko ya plastiki inatokomezwa.

Amesema Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeendelea kufanya juhudi mbalimbali kutoa elimu kwa umma juu ya athari za matumizi ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku, ambapo kwa kipindi cha miaka minne NEMC imefanya vipindi 88 vya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari, pamoja na kufanya mikutano 20 ya wadau mbalimbali kuhusu madhara ya matumizi ya mifuko ya plastiki.

Dkt. Semesi ameeleza kuwa katika kuhakikisha udhibiti wa matumizi ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku, NEMC katika kipindi cha miaka minne imefanya ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

“Kaguzi zimefanyika katika maeneo 178, ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki, ambapo maeneo 57 yalikutwa na makosa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria” ameeleza Dkt. Semesi.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW