China yaapa kupambana hadi mwisho dhidi ya ushuru wa Rais Trump

Na Dominic Allen

China imesema kuwa haitokubali kushurutishwa na Marekani kufuatia vita vya kibiashara vilivyochochewa na ushuru uliyowekwa na Rais Donald Trump kwa bidhaa zinazoingia nchini Marekani, jambo lililopelekea kuyumba kwa masoko ya hisa.

Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Wentao ametoa msimamo huo leo baada ya Rais Trump kutishia kuongeza ushuru kwa zaidi ya asilimia 100 kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani kutoka kwenye taifa hilo ambalo ni la pili kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani, ikiwa ni kujibu uamuzi wa Beijing wa kuweka ushuru wa ‘kisasi’ dhidi ya bidhaa za Marekani, kufuatia hatua ya awali ya Trump aliyotangaza juma lililopita.

“Kitisho cha Marekani kuongeza ushuru dhidi ya China ni kosa juu ya kosa, na kwa mara nyingine kinadhihirisha tabia ya ushurutishaji ya Marekani,” amesema Wentao

“Marekani ikisisitiza kutekeleza matakwa yake, China itapigana hadi mwisho,” ameongeza Wentao

Kwa upande wa wawekezaji na viongozi wa kisiasa ulimwenguni wamekuwa wakihangaika kuelewa kama ushuru wa Rais Trump ni wa kudumu au ni mbinu ya shinikizo ili kupata ustahimilivu kutoka kwa nchi nyingine.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW