Dr. Kahyoza: Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi, maendeleo ya kiuchumi Tanzania

Na Dr. Bravious Kahyoza

Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi, moja ya miradi mikubwa ya miundombinu nchini Tanzania, ambao ulianza kutekelezwa Februari 25, 2020 wakati wa uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli, na kukamilishwa kwa asilimia 75 chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Daraja hili, lenye urefu wa kilomita 3.2 na upana wa mita 28, limegharimu dola za Marekani milioni 300 (sawa na Shilingi za Kitanzania trilioni 0.78) zilizotokana na fedha za ndani.

Daraja la Kigongo-Busisi lililozinduliwa mkoani Mwanza mnamo Juni 19, 2025, limejengwa ili kuunganisha maeneo ya Kigongo mkoani Mwanza pamoja na Busisi mkoani Simiyu, likipunguza changamoto za usafiri wa feri ambazo zimekuwa zikizuia harakati za watu na bidhaa katika eneo hili. Kwa urefu wa kilomita 3.2, daraja hili limekuwa refu zaidi la aina yake katika eneo la Afrika Mashariki, likiwa na uwezo wa kubeba magari mazito na kuhimili mzigo wa tani 180. Upana wa mita 28 unaruhusu magari 1,600 kupita kwa wakati mmoja, na hivyo kuimarisha ufanisi wa usafiri wa barabarani.

Ujenzi wa daraja hili umefadhiliwa kwa fedha za ndani, ikiashiria uwezo wa Tanzania wa kujiendesha kiuchumi bila kutegemea misaada ya nje. Hii ni hatua ya maana katika kuhakikisha uhuru wa kiuchumi na uendelevu wa miradi ya miundombinu. Utekelezaji wake umefanywa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation ikishirikiana na China Railway 15 Bureau Group Corporation (CCECC – CR15G JV), chini ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).

Kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2019 na Global Facility for Disaster Reduction and Recovery (GFRR), uwekezaji wa dola moja ($1) katika miradi ya miundombinu kama daraja au barabara katika nchi zinazoendelea kama Tanzania unazalisha dola za Marekani Nne kwenye Pato la Taifa (GDP). Kwa kuwekeza dola za Marekani milioni 300 kwenye Daraja la Kigongo-Busisi, Tanzania inatarajiwa kuchangia dola za Marekani bilioni 1.2 (sawa na Shilingi Kitanzania trilioni 3.12) kwenye Pato la Taifa.

Ongezeko hilo litaimarisha uchumi wa Taifa kupitia maendeleo ya kibiashara, ambapo daraja litapunguza gharama na wakati wa usafiri kati ya Mwanza, Simiyu na mikoa mingine, na hivyo kuwezesha wafanyabiashara hasa wale wanaoshiriki katika kilimo, uvuvi na biashara ndogo ndogo.

Vilevile ujenzi wa daraja umetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi wa ndani, pamoja na ajira za muda mrefu katika sekta za usafirishaji, biashara na huduma zinazohusiana na daraja hili, huku likitarajiwa kuimarisha mtandao wa usafirishaji wa barabarani kwa kuunganisha maeneo ya kibiashara, viwanda na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Juhudi za Rais Samia katika kuimarisha miundombinu

Chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Awamu ya Sita imezingatia uwekezaji katika miundombinu ya msingi ili kukuza uchumi wa Taifa. Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi ni sehemu ya mipango mikubwa ya Serikali ya kuboresha miundombinu ya usafirishaji, ikiwa ni pamoja na barabara, viwanja vya ndege na bandari.

Jitihada hizi zimechukua mwelekeo wa kipekee wa kutumia rasilimali za ndani, kama ilivyoonekana katika ujenzi wa daraja hili. Aidha, Serikali imefanya kazi kwa ushirikiano na wadau wa ndani na kimataifa kuhakikisha ujenzi wa daraja hili unakamilika kwa wakati na kwa ubora wa juu. Hii inaonyesha dhamira ya Rais Samia ya kuimarisha miundombinu na kukuza uchumi endelevu.

Daraja la Kigongo-Busisi linatarajiwa kuchangia pakubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania. Mbali na kutazamiwa kuchangia Shilingi za Kitanzania trilioni 3.12 kwenye Pato la Taifa, daraja hili pia litasaidia kuongeza ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Mwanza na Simiyu pamoja na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa Victoria.

Gharama za Usafirishaji pia zitapungua, kwani badala ya kutegemea feri, ambazo mara nyingi zimekuwa zikichelewesha usafirishaji, daraja hili litapunguza gharama na wakati wa kusafirisha bidhaa na watu.

Miundombinu iliyoboreshwa itavutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa, hasa katika sekta za kilimo, uvuvi, na utalii, ambazo zinategemea usafirishaji wa haraka na wa uhakika. Bila kusahau kuwa maeneo ya Busisi na mengine yanayozunguka daraja hili yatapata fursa za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na ukuaji wa Biashara ndogo, hoteli, na huduma za usafirishaji.Pindi litakapokamilika, Serikali inatarajia kuimarisha usimamizi wa daraja hili kupitia taasisi kama vile Wakala wa Barabara (TANROADS), ili kuhakikisha linaendelea kutoa huduma za uhakika na kusaidia uchumi kwa miongo kadhaa ijayo.

Kukamilika kwa asilimia 75 Daraja la Kigongo-Busisi, ni ushahidi wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kukuza miundombinu na uchumi wa Tanzania. Juhudi hizi za Serikali za Awamu ya Sita zinaonyesha jinsi uwekezaji wa ndani unavyoweza kuleta maendeleo endelevu, na kuifanya Tanzania kuwa kielelezo cha maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.

Mwandishi: Dr. Bravious Kahyoza

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW