Mhagama: Prof. Janabi anatosha Ukurugenzi WHO Kanda ya Afrika

Na Wizara ya Afya

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema Prof. Mohamed Janabi ni mtu sahihi ambaye anaweza kuongoza Sekta ya Afya Kanda ya Afrika kutokana na uzoefu wake.

Mhagama amesema hayo Machi 22, 2025 Jijini Dodoma, katika mkutano wa waandishi wa habari ambao umelenga kutoa tamko rasmi la kumtambulisha Prof. Janabi na kuanza kwa kampeni ya kumnadi mgombea wa Tanzania ambaye atachuana na wagombea wengine watatu.

“Zipo sababu nyingi za Prof. Janabi kuwa Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, miongoni mwa hizo ni Diplomasia ya nchi yetu kimataifa ambayo Rais wetu wa awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitengeneza kimataifa na kuwezesha mataifa mengine kutambua weledi wetu kwenye sekta ya Afya” amesema Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amesema Prof. Janabi aliongoza mageuzi makubwa katika huduma za matibabu ya moyo nchini Tanzania na barani Afrika na hivyo kuwezesha kupunguza rufaa za nje ya nchi kwa asilimia 95 hali inayotoa taswira kuwa anaweza.

Mhagama ameongeza kuwa, Prof. Janabi amefanya kazi kwa ukaribu na Mashirika ya Kikanda, Kimataifa, Serikali mbalimbali Barani Afrika na Ulimwenguni kote pamoja na Wadau wa Sekta ya Afya ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora na endelevu za afya.

“Uzoefu wake wa kitaaluma na kiutendaji unampa sifa zinazohitajika kuongoza Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika kwa ufanisi mkubwa” amefafanua Waziri Mhagama.

Mhagama amesema ni wakati sahihi wa nchi kusimama na Mgombea wake ambaye mbali na kuhudumu kwenye Sekta tofauti pia Prof. Janabi amekuwa mshauri wa karibu wa Viongozi wa juu akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na sasa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika imempendekeza Prof. Mohamed Yakub Janabi, ambaye ni Mshauri wa Rais kwenye masuala ya afya na lishe kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika.

Mhagama ameongeza kuwa Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi tatu (3) kati ya 47 zilizosimamisha wagombea kwenye kinyang’anyiro hicho kitakachofanyika Mei 18, 2025 Geneva Uswisi.

Prof. Janabi anaingia katika uchaguzi huo akishindana na wagombea wengine watatu ambao ni: Profesa Moustafa Mijiyawa (Togo), Dkt. Michael Yao (Ivory Coast) na Dr. Mohamed Lamine Drame (Guinea Conakry) ili kuziba nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo, Dk. Faustine Ndugulile, waziri wa wa zamani wa afya Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 27, 2024.

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW