Huduma za upasuaji kwa watoto zaboreshwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya

Na Amiri Kilagalila

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imefungua huduma za chumba cha upasuaji wa watoto (Pediatric Operating Theatre) baada ya kufanyiwa maboresho makubwa na kuwekewa vifaa tiba vya kisasa.Maboresho hayo yamefanyika kwa ushirikiano wa Shirika la Kimataifa la Smile Train kutoka Marekani linaloratibu matibabu ya mdomo wazi na Shirika la Kids Operating Room (KidsOR) kutoka nchini Scotland linalojitolea kuboresha huduma za afya ya watoto kupitia uwekezaji kwenye miundombinu ya upasuaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana Mei 05, 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Uwesu Mchepange amewashukuru wafadhili kwa msaada wao na kubainisha kuwa maboresho hayo yataongeza ufanisi wa utoaji huduma za upasuaji kwa watoto, ambapo pia yameunda mazingira rafiki na ya kuvutia kwa watoto wanaopata huduma za upasuaji yatakayosaidia kupunguza hofu kabla na baada ya upasuaji.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau wamefanya maboresho haya makubwa kwenye vyumba vya upasuaji kwa ajili ya huduma za watoto, vyumba hivi sasa ni rafiki kwa ajili ya kutoa huduma kwa maana mazingira yake kuwa rafiki lakini kuwekewa vifaa vya kisasa kabisa” amesema Dkt. Mchepange.

Chumba cha upasuaji kwa watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kikiwa kimefanyiwa maboresho makubwa na kuwekewa vifaa vya kisasa. Picha na Amiri Kilagalila.

Dkt. Mchepange pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa nafasi kwa wadau wa maendeleo kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Moja ya mashine za kisasa ndani ya chumba cha upasuaji kwa watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya tayari kwa kutoa huduma za upasuaji zenye ufanisi na usalama kwa watoto. Picha na Amiri Kilagalila.

Kwa upande wake, Veronica Kimwela, Msimamizi wa Miradi ya Smile Train Tanzania pamoja na Jenn Perkison Mratibu wa KidsOR, wameishukuru hospitali hiyo kwa kutoa nafasi ya kushirikiana nao katika mradi huo muhimu, na kuahidi kuwa mashirika hayo yataendelea kushirikiana na hospitali hiyo na taasisi nyingine za afya nchini kwa manufaa ya watoto wa Tanzania.

“Kwa muda mrefu sana tumekuwa tukishirikiana na hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya na kutokana na mahusiano mazuri tuliyokuwa nayo tumeweza kuwaletea chumba cha upasuaji cha watoto wadogo na tunaamini chumba hiki kitaleta mabadiriko kwa watoto wote watakaokuja kutibiwa” amesema Veronica Kimwela.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Uwesu Mchepange (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi hospitali hiyo, wawakilishi wa Shirika la Smile Train na kidsOR na viongozi wengine wakati wa uzinduzi wa chumba cha upasuaji kwa watoto kilichofanyiwa maboresho. Picha na Amiri Kilagalila.

Ufunguzi wa chumba cha upasuaji wa watoto kilichofanyiwa maboresho unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kutoa huduma bora za upasuaji kwa watoto kutoka nyanda za juu kusini na maeneo mengine ya jirani na kufanya hospitali hiyo kupiga hatua kubwa katika kuboresha afya za watoto nchini Tanzania.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW