Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, ametoa wito kwa mataifa yote duniani kuunganisha nguvu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda mazingira.
Rais Erdoğan ametoa wito huo alipokuwa akihutubia viongozi wa dunia katika Mkutano wa Viongozi wa COP31 Antalya nchini Uturuki huku yeye akiwa mwenyeji wa mkutano huo ikiwa leo Novemba 11 ni siku ya tatu tangu kuanza kwake Novemba 9, 2026.
Mkutano huo muhimu wa COP31 umewakutanisha wakuu wa nchi na wajumbe mbalimbali ili kujadili hatua madhubuti za kuokoa sayari ya Dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira.
Katika hotuba yake, Rais Erdoğan amesisitiza kuwa wanadamu wote wanaishi katika nyumba moja yenye paa moja ambalo ni anga, na bustani moja ambayo ni Dunia huku akionya kuwa hakuna anga lingine, Dunia nyingine, bahari, wala misitu mingine mbadala endapo mazingira ya sasa yataharibiwa.
Lengo kuu la wito huo ni kuhakikisha kuwa mkutano wa COP31 unakuwa wa utekelezaji kwa vitendo badala ya kubaki kwenye ahadi pekee.
Uturuki imesisitiza kuwa kulinda dunia ni jukumu la pamoja linalohitaji maamuzi ya haraka na uwajibikaji wa kila taifa kwa manufaa ya vizazi
#COP31 #mazingira #Uturuki #utekelezaji


