Rais Samia kuwasili Uturuki kushiriki mkutano wa COP31

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuondoka leo, Novemba 10, 2026, nchini Tanzania kuelekea mjini Antalya, Uturuki, kushiriki Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).

Mkutano huo ulianza jana, Novemba 9, 2026, ukiwa na ajenda mbalimbali zinazohusu mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo afya, usalama wa chakula na kilimo.

Katika ziara hiyo, Rais Samia pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo.

Mkutano  huo, unawakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali, wanadiplomasia, wataalamu wa mazingira, wanasayansi na mashirika ya kiraia ili kujadili changamoto mbalimbali zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi duniani, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na athari zake.

COP ni mkutano wa kila mwaka unaofanyika chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC), ulioanzishwa mwaka 1992. Huu ni mkutano wa 31 tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo, ambalo limekuwa sehemu muhimu ya majadiliano ya kimataifa kuhusu kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuweka mikakati ya ufadhili wa miradi ya kukabiliana na changamoto hizo.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW