Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo hii leo amekamatwa na watu ambao hawajafahamika hadi sasa maeneo ya Stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi Louis jijini Dar es Salaam.
Taarifa kutoka chama cha ACT Wazalendo imesema kuwa, majira ya saa 11 alfajiri leo, Nondo alifika katika kituo hicho cha mabasi kwa ajili ya usafiri wa basi la Saratoga lenye namba za usajili T 221 DKB, ambapo watu waliokuwa na gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 249 CMV, walimkamata kwa nguvu jambo lililopelekea vitambulisho vya Abdul Nondo kudondoka pamoja na pingu alizokuwa amebeba mmoja wa watu hao kudondoka.
Hata hivyo msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime amesema kuwa wamepata taarifa hizo na wanafuatilia tukio hilo, sambamba na kufungua jalada.


