Na Yohani Gwangway
Zaidi ya wajumbe 1,000 wa Mkutano Mkuu wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 21 mwezi huu.
Kiu ya wengi imekuwa ni kufahamu idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho watakaopiga kura kuamua nani anaongoza chama hicho katika ngazi ya Taifa katika uchaguzi unaovuta hisia za wengi kutokana na ushindani ulipo kati ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu wanaowania nafasi ya Uenyekiti Taifa.
Kwa mujibu wa katiba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya mwaka 2006 na Marekebisho yake ya mwaka 2019, Ibara ya 7.7.8 inataja Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho ambao watapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao. Wajumbe hao ni kama ifuatavyo;
- Wajumbe wote wa Kamati Kuu
- Wajumbe wote wa Baraza Kuu
- Wenyeviti wa Wilaya/ Majimbo
- Makatibu wa Wilaya/Majimbo
- Wajumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
- Wajumbe 20 wa Mikutano Mikuu kutoka kila Baraza(BAZECHA, BAVICHA na BAWACHA)
Wajumbe 5 wa Baraza Kuu kutoka kila baraza - Mjumbe Mwakilishi wa kila Wilaya
- Viongozi wa Kitaifa wa Mabaraza ambao siyo wajumbe wa Kamati Kuu
JEDWALI LA 1: Makundi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA

Land Dwellers imefanya majumuisho kutoka Kanda 10 za CHADEMA, ambapo zaidi ya wajumbe 1,000 watapiga kura katika uchaguzi huo wa tarehe 21 mwezi huu. Kwa mujibu wa taratibu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wajumbe hawa watatoka katika maeneo yafuatayo;
- Wajumbe 4 kutoka kila kanda kutoka kanda 10 za chadema
- Wajumbe 2 kutoka kila mkoa, kutoka mikoa 34 ya kichama
- Wajumbe 2 kutoka kila wilaya kutoka wilaya 81 za chama
- Wajumbe 3 kutoka kila jimbo, kutoka majimbo 264 ya chama
- Jumla ya wajumbe 92 wa Mabaraza ( BAZECHA, BAWACHA na BAVICHA)
JEDWALI LA 2: Idadi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Majimbo ya CHADEMA nchi nzima

Wajumbe 4 kutoka Kanda ni;
- Mwenyekiti wa Kanda
- Makamu Mwenyekiti wa Kanda
- Katibu wa Kanda
- Mweka hazina wa Kanda
Kuna Kumla ya Kanda 10 za CHADEMA. Kanda ya Unguja haijafanya uchaguzi, kwahiyo kutakuwa na wajumbe 36 wa Mkutano Mkuu kutoka kanda 9 zilizofanya uchaguzi.
Wajumbe 2 wa Mkutano Mkuu kutoka kila mkoa ni;
- Mwenyekiti wa chama Mkoa
- Katibu wa chama Mkoa
Kuna jumla ya mikoa 34. Mkoa wa Njombe utakosa kura ya Mwenyekiti wa Mkoa kwa sasabu uchaguzi huo ulishindikana katika nafasi hiyo pekee. Kwa maana hiyo kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka katika mikoa 34 itakuwa 67 baada ya kutoa mjumbe mmoja wa Mkoa wa Njombe.
Wajumbe 2 wa Mkutano Mkuu kutoka kila Wilaya ni
- Mwenyekiti wa chama Wilaya
- Katibu wa chama Wilaya
CHADEMA ina jumla ya Wilaya 81. Wilaya 5 hazijafanya uchaguzi. Idadi wajumbe itapungua kutoka 162 hado 172 kutokana na maeneo ambayo hayajafanya uchaguzi. Katika eneo hili ni muhimu kuelewa kuwa baadhi ya kura chache zinaweza kupungua kwa sababu baadhi ya wajumbe wanashika nafasi mbili za uongozi lakini kura zao haziwezi kuhesabiwa mara mbili.
Wajumbe 3 kutoka jimbo ni
- Mwenyekiti wa chama Jimbo
- Katibu wa chama Jimbo
- Mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka jimbo husika
CHADEMA ina majimbo 264. Kati ya majimbo haya majimbo 21 hayajafanya uchaguzi. Kwa hiyo wajumbe 63 kutoka majimbo hayo hawataweza kuwa sehemu ya Mkutano Mkuu wa chama. Hivyo kutakuwa na wajumbe 729 kutoka majimbo 243 yaliyofanya Uchaguzi. Kura zitakazopungua kwa sababu ya wajumbe kuwa na nafasi zaidi ya moja ya uongozi zinatarajiwa kuwa chache katika eneo hili.
JEDWALI LA 3: Idadi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na majimbo ambayo hayajafanya uchaguzi

Wajumbe kutoka Mabaraza ya Chama
Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA kila Baraza litatoa wajumbe wa Mkutano Mkuu kutokana na muundo wake. Kutoka Mabaraza haya ni Baraza la Wazee la CHADEMA (BAZECHA), Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) na Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA). Mabaraza yote kura za Mwenyekiti na Katibu wa Baraza husika halitatoka kwao ili kuepusha kura mara mbili kwa sababu viongozi hao pia ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) ni;
- Wajumbe 20 wa Mkutano Mkuu wa BAVICHA
- Wajumbe 5 wa Baraza Kuu la BAVICHA
- Viongozi 6 wa BAVICHA tofauti na Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu Taifa
Viongozi hawa 6 ni;
- Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA bara
- Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Zanzibar
- Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA bara
- Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA Zanzibar
- Mweka hazina wa BAVICHA Taifa
- Katibu wa Uenezi na Uhamasishaji wa BAVICHA Taifa.
Kwa maana hiyo kutoka BAVICHA kutakuwa na jumla ya wajumbe 31 wa Mkutano Mkuu Taifa.
Wajumbe wa mkutano mkuu kutoka Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) ni;
- Wajumbe 20 wa Mkutano Mkuu wa BAWACHA
- Wajumbe 5 wa Baraza Kuu la BAWACHA
- Viongozi 6 wa BAWACHA tofauti na Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu Taifa
Viongozi 6 wa kitaifa wa BAWACHA ni;
- Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA bara
- Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Zanzibar
- Naibu Katibu Mkuu wa BAWACHA bara
- Naibu Katibu Mkuu wa BAWACHA Zanzibar
- Mweka hazina wa BAWACHA Taifa
- Katibu wa Uenezi na Uhamasishaji wa BAWACHA Taifa.
Kwa upande wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) kutakuwa na jumla ya wajumbe 31 wa Mkutano Mkuu.
Kwa upande wa Baraza la Wazee la Wazee la CHADEMA (BAZECHA), Wajumbe wa mkutano Mkuu watakuwa;
- Wajumbe 20 wa Mkutano Mkuu wa BAWACHA
- Wajumbe 5 wa Baraza Kuu la BAWACHA
- Viongozi 5 wa BAWACHA tofauti na Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu Taifa
- Makamu Mwenyekiti wa BAZECHA bara
- Makamu Mwenyekiti wa BAZECHA Zanzibar
- Naibu Katibu Mkuu wa BAZECHA bara
- Naibu Katibu Mkuu wa BAZECHA A Zanzibar
- Mweka hazina wa BAZECHA Taifa
Kutoka BAZECHA kutakuwa na Jumla ya wajumbe 31 wa Mkutano Mkuu.
Ukiachana na wajumbe hawa, wajumbe wengine watakuwa ni wajumbe 8 kutoka Kamati Kuu ya chama hicho wanaochaguliwa na Baraza Kuu la Chama. Kuna makundi mengine ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu. Land Dwellers itaendelea kutafuta taarifa za jumla ya wajumbe wote wa Kamati Kuu ambao kikatiba wanatakiwa kupiga kura katika Mkutano Mkuu ujao.
Majumuisho ya kila Kanda
Land Dwellers imefanya majumuisho wa takwimu kutoka Kanda zote za CHADEMA nchi nzima na kukuletea idadi ya wajumbe kutoka kila Kanda. Katika takwimu hizi idadi ya wajumbe iliyopo ni ile iliyotakiwa kikatiba bila kutoa wale ambao wamehama, wanashika nafasi mbili za uongozi au labda uchaguzi haujafanyika katika eneo husika.
Katika uchaguzi unaoonekana kuwa wa mvuto kuwahi kutokea katika chama hicho, kura nyingi zitakazoamua zitatokana na wajumbe wanaotokana na majimbo ambao ni zaidi ya 700 nchi nzima. Wajumbe wengine watakaokuwa na nafasi kubwa ya maamuzi ni wajumbe wanaowakilisha wilaya ambao ni zaidi ya 150 nchi nzima. Wajumbe wa mabaraza nao watakuwa na nguvu kwani watakuwa zaidi ya 90. Makadirio haya ni kwa sababu baadhi ya wajumbe hawatashiriki kwa sababu maeneo yao hayajafanya uchaguzi au sababu nyinginezo.
JEDWALI LA 4: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Unguja

JEDWALI LA 5: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Serengeti

JEDWALI LA 6: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Pwani

JEDWALI LA 7: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Pemba

JEDWALI LA 8: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Nyasa

JEDWALI LA 9: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Magharibi

JEDWALI LA 10: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Kusini

JEDWALI LA 11: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Kati

JEDWALI LA 12: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Kaskazini

JEDWALI LA 13: Idadi ya Mikoa, Wilaya, Majimbo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa Kanda ya Victoria

Muhimu: Kuna wajumbe katika baadhi ya maeneo wamehama, wamefariki au hawataweza kuwepo katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA, hivyo kuathiri idadi ya wajumbe watakaopiga kura katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Januari 21, 2025.
Mwandishi : Yohani Gwangway
Mhariri: Dominic Allen


