Mwabukusi awataka viongozi wa dini kuwafukuza wakandamizaji kanisani

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Anyisile Kajunjumele Mwabukusi, amesema miongoni mwa mambo anayoyakumbuka kuhusu marehemu Wakili Alute Mughwai Lissu, kaka mkubwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ni msimamo wake wa kutosema uongo mbele ya hadhara, akieleza kuwa kila jambo alilokuwa akilitamka lilikuwa na ukweli ndani yake.

Mwabukusi amesema kuwa misingi inayowafurahisha baadhi ya watawala imekuwa ikihusisha uchawa, uongo, urafi, wizi wa mali za umma, ukandamizaji pamoja na vitendo vya kuvunjwa na kuvurugwa kwa Katiba. Ameeleza kuwa hali hiyo imewafanya baadhi ya watu kuogopa kusema ukweli, lakini amesisitiza kuwa wao wataendelea kuusema ukweli wakati wowote, unaofaa na usiofaa, kwa kuwa Mungu wanayemwamini ni wa kweli.

Kuhusu hatua za kisheria zinazomhusu Tundu Lissu, Mwabukusi amesema watashirikiana na mawakili wake kwa kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Lissu mwenyewe.

Amesema Kuhusu hatua za kisheria zinazomhusu Tundu Lissu, Mwabukusi amesema watashirikiana na mawakili wake kwa kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Lissu mwenyewe. Amesema kwa kushirikiana na baraza la uongozi pamoja na timu ya mawakili, watahakikisha suala la rufaa linashughulikiwa kwa haraka, sambamba na kufuatilia maombi ya dhamana wakati wakisubiri rufaa hiyo kusikilizwa.

Aidha, amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla kutowapa nafasi watu wanaoshiriki katika vitendo vya ukandamizaji ndani ya taasisi za dini na kuwaasa viongozi wa dini kuwafukuza kanisani na kutowapatia sakramenti watu wanaohusika na ukandamizaji, akieleza kuwa ni muhimu kuhoji namna watu wanaotoa hukumu zinazopotosha haki wanavyoweza kuendelea kushiriki katika shughuli za kidini.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW