Watu 13 wamepoteza maisha na wengine 84 wameokolewa kufuatia kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Dar es Salaam Novemba 16, 2024.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na wananchi kwa njia ya vyombo vya habari akiwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Samia amesema kuwa serikali itabeba gharama za matibabu kwa majeruhi na mazishi kwa waliopoteza maisha kufuatia kuanguka kwa ghorofa Kariakoo, Dar es Salaam.

Hata hivyo Rais Samia amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongozana na wakaguzi wa majengo kukagua majengo eneo lote la Kariakoo ili kupata taarifa kamili ya majengo hayo, huku akilitaka Jeshi la Polisi Tanzania kupata taarifa kamili ya jengo lililoporomoka.


