
Tundu Lissu, mwanasiasa maarufu wa upinzani na kiongozi wa CHADEMA, amepatikana na hatia ya kosa la uchochezi katika uamuzi uliotolewa na Mahakama kuu-Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Hukumu hiyo imesomwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Jaji James Karayemaha pamoja na Jaji Ferdinand Kiwonde, katika kesi ya uhaini iliyosajiliwa kwa Namba 19605/2025.
Uamuzi huo ukisomwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Mahakama imeridhika kuwa ushahidi wote uliowasilishwa mahakamani hapo umejikita kwenye kosa la uchochezi badala ya kosa la uhaini linalobeba adhabu ya kifo.

