Watu 98 wafariki dunia baada ya paa la ukumbi kuanguka Santo Domingo

Na Dominic Allen

Takribani watu 98 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 160 wamejeruhiwa baada ya kuanguka kwa paa la ukumbi wa starehe wa Jet Set uliyopo katika mji mkuu wa Santo Domingo nchini Jamhuri ya Dominika.

Mamlaka nchini humo zimesema kuwa paa la ukumbi huo lilianguka mapema hapo jana wakati wa Tamasha la Merengue lililohudhuriwa na wanasiasa, wanamichezo na wengineo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Operesheni za Dharura, Juan Manuel Méndez jana usiku alisema kuwa bado vikosi vya uokoaji vinaendelea na zoezi la kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.

“Tunaendelea kuondoa mabaki na kuwatafuta watu…Tutatafuta watu bila kuchoka” alisema Méndez.

Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Gavana wa jimbo la kaskazini-magharibi la Montecristi, Nelsy Cruz pamoja na mwanamichezo wa zamani wa Major League Baseball, Octavio Dotel mwenye umri wa miaka 51 ambaye alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitalini baada ya kuokolewa kutoka kwenye kifusi.

Kwa mujibu wa mamlaka nchini humo wakati ajali hiyo inatokea, mamia ya watu walikuwa ndani ya ukumbi huo, ambapo kuna hofu huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW