Israel na Hamas kubadilishana wafungwa kwa mateka kwa mara ya pili

Na Dominic Allen

Israel na kundi la Hamas wanatarajia kubadilishana wafungwa kwa mateka hii leo, haya yanakuwa mabadilishano ya pili tangu pande hizo mbili kufikia muafaka wa kusitisha mapigano yaliyodumu kwa miezi 15 huko Gaza.

Katika mabadilishano yatakayofanyika leo, wanajeshi wanawake wanne wa Israel wanaoshikiliwa mateka na Hamas wanategemewa kuachiliwa huku Israel ikitakiwa kuawaachia huru wafungwa Wapalestina 200 waliopo magerezani nchini humo, ikijumuisha wafungwa 120 ambao wanatumikia kifungo cha maisha kwa kufanya mashambulizi hatari nchini Israel.

Mateka wanaoshikiliwa na Hamas ni Karina Ariev, Daniella Gilboa, Naama Levy, na Liri Albag, wote hawa walikamatwa na Hamas katika shambulizi lililofanywa na kundi hilo Oktoba 7, 2023 ambalo lilipelekea kuzuka kwa vita hivyo.

Wanajeshi hao walichukuliwa kutoka kambi ya Nahal Oz karibu na mpaka wa Gaza wakati wanamgambo wa Kipalestina walipoivamia, wakiwaua zaidi ya wanajeshi 60 mahali hapo.

Wanajeshi waliotekwa wote walikuwa wanahudumu katika kikosi cha walinzi wa mipaka, ijapokuwa kuna mwanajeshi wa tano wa kike katika kikosi chao, Agam Berger, ambaye alitekwa pamoja nao lakini hakuorodheshwa katika orodha hiyo.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW