Wananchi Ulyankulu wampa kongole Rais Samia zoezi la Madaktari Bingwa

Na Wizara ya Afya

Wananchi wilayani Kaliua mkoani Tabora katika Kituo cha Afya Ulyankulu wamepongeza hatua ya serikali kupitia Wizara ya Afya kuwapelekea huduma ya Madaktari Bingwa kwenye kituo chao.

Pongezi hizo za wananchi zimetolewa Aprili 30, 2025 ikiwa ni siku pili ya kambi ya Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia katika eneo hilo ambalo limekuwa na uhitaji wa muda mrefu.

“Mara zote tumekuwa tukisikia kambi hii ya wataalam wetu wakija wilayani, lakini walikuwa hawajawahi kufika huku kwetu, hivyo tulikuwa tunashindwa kufika kwa sababu hatuna fedha za kwenda huko” amesema Bw. Slivesta Bahite mkazi wa kijiji cha Ikonongo.

Naye Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha afya, Dkt. Leonard Nyigo amesema, ndani ya siku mbili za huduma wananchi zaidi ya 200 wamejitokeza kwa ajili yakupata huduma za kibingwa.Dkt. Nyingo ameongeza kuwa, wataalam hao wamekuwa msaada mkubwa sio tu kwa ajili ya huduma lakini pia kuwajengea uwezo watumishi wa kituo hicho.

“Tumenufaika na ujio huu, kwakuwa umetuwezesha kuimarisha huduma zetu kama vile huduma ya NCU ambayo ilikuwa haijaanza lakini tulikuwa na vifaa, hivyo tunaishukuru sana serikali kwa kuona umuhimu” amesema Dkt. Nyigo.

Baadhi ya wananchi wakiwa katika Kituo cha Afya Ulyankulu, kwa ajili ya kupata huduma kutoka kwa Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia. Picha na Wizara ya Afya.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Dkt. Amos Charles amesema imekuwa tofauti sana na kambi zingine alizowahi kushiriki kwani ndani ya siku moja tu aliweza kuhudumia watoto 39, ambapo kwa kawaida huhudumia watoto kati ya 15 hadi 20 wakati wa kliniki zingine.

Aprili 28, 2025 Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama alizindua mzunguko wa tano wa Kambi za Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia Suluhu Hassan na kuwaomba viongozi wa ngazi zote kuhamasisha wananchi kujitokeza ili kupatiwa huduma hiyo iliyobuniwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW