TASAF yamaliza kilio cha nyumba ya walimu, Manga

Na Amiri Kilagalila

Kufuatia changamoto ya upungufu wa nyumba ya walimu inayowakumba walimu wa Shule ya Msingi Deo Sanga iliyopo kijiji cha Manga katika Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho wanatarajia kukamilisha ujenzi wa nyumba pacha yenye thamani ya Tsh. Milioni 92.41.

Baadhi ya walimu hao wanaofundisha katika Shule ya Msingi Deo Sanga wamekuwa wakitembea umbali wa takribani kilomita 24 kila siku kutokana na kuishi mbali na shule hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF, Peter Ilomo (kulia) akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba pacha ya walimu wa Shule ya Msingi Deo Sanga. Picha na Amiri Kilagalila.

Liston Ngimilanga ambaye ni Afisa Mtendaji wa kijiji cha Manga, leo Aprili 30, 2025 akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF, Peter Ilomo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi, amesema kuwa ujenzi umefikia hatua ya umaliziaji ambapo mradi huo mpaka sasa umegharimu Shilingi 91.36.

“Katika kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi wa kijiji cha Manga, kijiji kilipokea fedha hizo kutoka serikali kuu kupitia TASAF kwa ajili ya ujenzi wa nyumba pacha, na hii ni baada ya wananchi kuibua na kuthibitisha mradi” amesema Ngimilanga.

Mradi wa nyumba pacha ya walimu wa Shule ya Msingi Deo Sanga ukiwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kutumiwa na walimu wa shule hiyo.

Nae Naboti Ilongo ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Deo Sanga, amesema mpaka sasa shule hiyo ina nyumba nne lakini mahitaji yao ni nyumba saba hivyo mara baada ya ujenzi wa nyumba hiyo kutakuwa na mahitaji ya nyumba moja.

Ilongo ameongeza kuwa baadhi ya walimu wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kusafiri umbali mrefu hadi kufika shuleni hapo wakitokea mjini Makambako.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF, Peter Ilomo amesema serikali imetoa kiasi hicho ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Manga ambapo amechukua nafasi hiyo kupongeza kwa usimamizi wa mradi huo.

“Jengo ni zuri na hata umaliziaji wake umefanyika kwa umahili mkubwa, na kwa kweli niwashukuru CMC kwa kusimamia hii kazi na nina imani mwezi ujao mtakuwa mmemaliza hii kazi” amesema Ilomo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF, Peter Ilomo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Manga, Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, wakati akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba pacha ya walimu wa Shule ya Msingi Deo Sanga. Picha na Amiri Kilagalila.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW