PAD yamtaka Rais wa Angola, Lourenço kuomba msamaha hadharani

Na Dominic Allen

Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD) limelaani vikali kitendo cha serikali ya Angola na Mamlaka zake kuwazuia kwenye Uwanja wa Ndege wa Luanda viongozi na wajumbe mbalimbali ambao waliwasili nchini hapo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika ambao ulifanyika hapo jana.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na PAD leo Machi 15, 2025 imeeleza kuwa sura halisi ya utawala wa Angola imefichuka, kwa kuwadhalilisha viongozi wa Afrika, Marais wa zamani pamoja na wapenda demokrasia.

PAD imemtaka Rais wa Angola, João Lourenço ajitokeze na aombe radhi hadharani kwa kuwazuia viongozi wa nchi za Afrika, wajumbe waliorudishwa nchini kwao pamoja na wote waliodhalilishwa na mamlaka za Angola.

Taarifa hii ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD) inafuatia baada ya viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika na nje ya Afrika kuzuiwa kuingia nchini Angola tangu Machi 13, 2025 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia uliyokuwa umepangwa kufanyika Benguela, Angola.

Miongoni mwa viongozi wa Tanzania waliozuiliwa  ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu pamoja na wajumbe wengine.

Baadhi ya Marais wa zamani pia walizuiliwa kuingia Angola, akiwemo Rais wa zamani wa Botswana, Ian Khama na Andre’s Pastrana Arango ambaye ni Rais wa zamani wa Colombia.

Kuzuiliwa kwa viongozi, wajumbe na wadau walienda nchini Angola kwa ajili ya kushiriki mkutano huo, kumezuia hisia kali kwa wapenda demokrasia wakisema kuwa kimetia doa dhana ya Umoja wa Afrika, kwa kuzingatia Rais wa Angola, João Lourenço ndiye Mwenyekiti wa umoja wa Afrika (AU).

Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD) limesema kuwa walioshikiliwa na Mamlaka za Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Luanda hawakuelezwa sababu ya kushikiliwa kwao. PAD inaamini kuwa kitendo hicho cha serikali ya Angola kimelenga kukwamisha  na kukandamiza maendeleo ya demokrasia barani Afrika.

Huu ni Mkutano wa tatu wa Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD) tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2023, ambapo huwaleta pamoja viongozi, watu mashuhuri na wadau mbalimbali kuzungumzia masuala yanayohusu demokrasia, na katika mkutano ulifanyika siku ya jana ulijadili mustakabali wa hali ya demokrasia barani Afrika.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW