Mtu mmoja akutwa na maambukizi ya virusi vya Marburg, Kagera

Na Dominic Allen

Mtu mmoja amegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Marburg huko Biharamulo mkoani Kagera,Tanzania baada ya kupimwa kwa sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu ambao walikuwa wakihisiwa kuwa maambukizi ya virusi hivyo.

Taarifa ya maambukizi hayo zimetolewa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza katika mkutano na Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amesema hadi sasa serikali inafuatilia kwa ukaribu visa vya watu 25 wanaohisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Marburg ambavyo kwa hapa nchini Tanzania viligunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi March 2023.

Shirika la WHO kupitia Katibu Mkuu wake, Tedros Adhanom Ghebreyesus limetoa ufadhili wa dola za Kimarekani milioni 3 ili kuiwezesha Tanzania kukabiliana na ugonjwa huo.

Msisitizo juu ya maambukizi ya virusi vya Marburg unafuatia baada taarifa iliyotolewa na WHO siku kadhaa zilizopita kuhusu vifo vya watu nane ambao walishukiwa kuwa na maambukizi ya virus vya marburg, ambapo WHO iliitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi juu ya maambukizi ya virusi hivyo.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW