Miili ya watu 78 yatolewa mgodini Stilfontein, Serikali ya Afrika Kusini yalaumiwa.

Takribani miili 78 ya wachimbaji haramu wa madini imetolewa na manusura 166 wameokolewa katika mgodi wa dhahabu huko Stilfontein, Afrika ya Kusini ambako polisi walizuia chakula na maji kwa miezi kadhaa jambo ambalo limepingwa vikali na vyama vya wafanyakazi vikisema kuwa ni ukandamizaji na ukatili dhidi ya watu waliokuwa wakijaribu kujitafutia riziki.

Operesheni ya uokoaji ilianza Januari 13, 2024 baada ya amri kutoka Mahakamani nchini humo. Baadhi ya manusura waliookolewa wamedhohofika na kuchanganyikiwa, huku mamia ya wanaume wengine bado wamekwama katika mgodi huo umbali wa kilomita 2 chini ya ardhi.

Tangu mwezi Agosti, 2024 Jeshi la Polisi nchini Afrika ya Kusini lilizuia kupelekwa kwa chakula na maji kwenye mgodi huo mpaka Disemba, 2024 baada ya Mahakama kuruhusu wale wanajitolea kupeleka misaada kwa wachimbaji hao wanaojulikana kwa jina la ‘Zama Zama’.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Afrika ya Kusini, Athlenda Mathe amesema kuwa kitendo cha kupeleka misaada ya chakula kwa wachimbaji hao haramu, ni kuunga mkono uhalifu.

“Jukumu letu lilikuwa kupambana na uhalifu, na hilo ndilo hasa tumekuwa tukifanya…kwa kutoa chakula, maji, na mahitaji muhimu kwa wachimbaji hawa haramu, polisi wangekuwa wanakubali na kuruhusu uhalifu kushamiri” alisema Athlenda.

Hatua hiyo ya kuwanyima chakula na maji wachimbaji hao imepingwa vikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Afrika Kusini.

“Wachimbaji hawa, wengi wao wakiwa wafanyakazi wasio na nyaraka na waliokata tamaa kutoka Msumbiji na nchi nyingine za Kusini mwa Afrika, waliachwa wafe” limesema Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Afrika Kusini katika taarifa yake hapo jana.

Chama cha siasa cha Democratic Alliance, ambacho ni cha pili kwa ukubwa nchini humo hi leo kimesema kuwa hali katika mgodi huo imekuwa “mbaya kupita kiasi” na kikatoa wito wa kufanyika uchunguzi huru.

Jeshi la Polisi limesema kuwa manusura wote 166 waliookolewa hadi sasa walikamatwa mara moja na kushtakiwa kwa makosa ya jinai yakiwemo uhamiaji haramu, kuingia bila ruhusa, na uchimbaji haramu, hakuna aliyelazwa hospitalini wote waliwekwa kizuizini na polisi.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW