Mapigano yashika kasi nje ya mji Goma, wananchi washauriwa kuhama

Na Dominic Allen

Hali imezidi kuwa tete nje ya mji wa Goma baada ya mapigano kuzuka hapo jana kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wanamgambo wa kundi la M23. Kufuatia mapigano hayo mataifa ya Uingereza, Marekani na Ufaransa yamewahimiza wakazi wa maeneo hayo kuondoka kwa sababu hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Tangu mazungumzo ya amani kushindikana kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na M23, katika siku za hivi karibuni kundi hilo limechukua maeneo makubwa katika sehemu za mashariki mwa nchi hiyo yenye utajiri wa madini, hali iliyosababisha mgogoro wa kibinadamu na pamoja kuuzingira maeneo hayo ambayo ni makazi ya watu milioni moja.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa (UN) ulionya kuwa mzozo unaoendelea katika jimbo la Kivu Kaskazini pia umesababisha zaidi ya watu 400,000 kukimbia makazi yao mwaka huu, na kutahadharisha kuwa unaweza kuchochea vita vya kikanda.

“Idadi ya watu waliolazimika kuhama sasa imezidi 400,000 mwaka huu pekee, karibu mara mbili ya idadi iliyoripotiwa juma lililopita.” alisema Matthew Saltmarsh, msemaji wa shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva hapo jana.

Kufuatia mizozo inayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), vyanzo vya kuaminika vililiambia Shirika la Habari la AFP kuwa tayari serikali ya nchi hiyo imeomba kufanya kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo bado hajafahamika ni lini kikao hicho kitafanyika.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW