Marekani yakosolewa kuchukua Ukanda wa Gaza

Na Dominic Allen

Baadhi ya Wamarekani wenye asili ya Kiarabu pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Marekani wamekosoa hatua ya nchi hiyo kutaka kuchukua eneo la Ukanda wa Gaza.

Miongoni mwa wakosoaji wa mpango huo ni Bishara Bahbah, mwanzilishi wa Shirika la Arab American for Peace aliyemuunga mkono Rais Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2024, alionesha kutofurahishwa na hatua hiyo ya Trump kutaka kuchukua Ukanda wa Gaza.

“Tunapinga uhamishaji wowote wa Wapalestina, iwe wa hiari au wa kulazimishwa, kutoka katika nchi yao.” Alisema Bahbah katika mahojiano na shirika la habari la Reuters.

Licha ya ukosoaji huo, Bahbah ameonekana kuwa imani kwa Rais Trump, akisema bado anamuunga mkono kwa sababu ni chaguo sahihi zaidi katika kutatua mgogoro huko Gaza, akibainisha kuwa alibadilisha hata jina la shirika alilolianzisha kutoka ‘Arab Americans’ na kuwa ‘Arab Americans for Peace’ siku mbili zilizopita, kuonyesha mwelekeo wake mpya kufuatia ushindi wa Trump katika uchaguzi mwaka jana.

Rais Donald Trump siku ya Jumanne wakati wa mkutano wa waandishi wa habari katika Ikulu ya White House pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliweka wazi mpango wa Marekani kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza.

Trump pia alipendekeza kuwahamisha Wapalestina kwenda katika nchi jirani na kuendeleza upya eneo hilo lililoharibiwa na vita, akisema kuwa Marekani italiendeleza eneo hilo kiuchumi, kujenga nyumba za kuishi pamoja na kutoa ajira.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW