Mahakama Kuu ya Uganda kuamua juu ya uhalali wa Mahakama za Kijeshi kuhukumu raia

Na Dominic Allen

Mahakama Kuu nchini Uganda hii leo itafanya maamuzi kuamua utata uliyopo kuhusu raia wa kawaida nchini humo kuhukumiwa na Mahakama za Kijeshi.

Jopo la Majaji saba likiongozwa na Jaji Mkuu, Alfonse Owiny Dollo litafanya maamuzi hayo kama ni sawa kwa Mahakama za Kijeshi kuhukumu raia wa kawaida au ni kinyume na Katiba ya Uganda.

Hatua hii imekuja baada ya aliyewahi kugombea nafasi ya Urais mara nne nchini humo, Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kukataa kuwasilisha utetezi wao mbele ya Mahakama Kuu ya Kijeshi huko Makindye jijini Kampala.

Besigye na Lutale wamekataa kufanya hivyo wakimesema kuwa wao siyo maafisa wa Jeshi la Uganda, hivyo hawapaswi kushtakiwa wala kuhukumiwa na Mahakama ya Kijeshi.

Ikumbukwe kuwa Kizza Besigye na Obeid Lutale walitekwa mnamo Novemba 16, 2024 walipokuwa jijini Nairobi, Kenya kwenye uzinduzi wa kitabu cha Martha Karua, baadae kupatikana nchini Uganda wakishikiliwa na vyombo vya usalama nchini humo, ambapo walifunguliwa kesi ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW