Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Odero Charles Odero ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hii leo.
Odero amesema tayari ameshaandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika kuhusu azma yake hiyo, na kuongeza kuwa ameamua kugombea kwa lengo la kuimarisha demokrasia, mshikamano na maendeleo ya taifa.
Mchakato wa uchaguzi wa nafasi ya Uenyekiti Taifa wa CHADEMA unatarajiwa kufanyika kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, ambapo Katiba ya chama hicho inaruhusu mwanachama yeyote kugombea nafasi hiyo.


