Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuporomoka kwa ghorofa, Kariakoo jijini Dar es Salaam imefika watu 20 hadi sasa.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 20, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na wananchi alipozulu eneo la tukio hilo ambapo amemtaka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongozana na timu ya wakaguzi wa majengo kwa ajili ya kukagua majengo yaliyopo Kariakoo na kuweka bayana majibu ya ripoti hiyo ili kudhibiti janga kama hilo lisitokee.

Katika hatua nyingine Rais Samia ametoa rai kwa wafanyabiashara wa maeneo ya karibu na jengo lililoporomoka kusitisha shughuli zao muda hadi pale hali itakapokuwa sawa.
Tangu kutokea kwa tukio hilo Novemba 16, 2024 zaidi watu 80 wamejeruhiwa huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu.


