DC Makete awaonya wakandarasi, “Msifanye mchezo”

Na Amiri Kilagalila

Mkuu wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Kissa Kasongwa amewaonya wakandarasi wanaofika na kutekeleza miradi chini ya kiwango wilayani humo, hali inayopelekea miradi hiyo kuharibika ndani ya muda mfupi na kusababisha kero kubwa kwa wananchi.

DC Kissa ametoa onyo hilo jana Juni 19, 2025 baada ya kusikiliza kero ya wakazi wa kijiji cha Isapulano katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji ambapo amesema amebaini changamoto ya kutopitika kwa barabara nyingi katika wilaya hiyo, hususani katika kipindi cha mvua na hilo limetokana na kupewa kazi wakandarasi wasiokuwa na uwezo.

“Changamoto kubwa niliyoikuta ni kwamba barabara nyingi hazipitiki, kwanza wanapewa wakandarasi ambao hawana uwezo, nimekaa na wakandarasi kuwaambia mmekuwa mkifanya mchezo na kufanya Makete sehemu ya kutafutia mitaji sasa ole wake mtu afanye kazi ya kutafutia mtaji hapa, nitashughulika na wao” amesema DC Kissa.

Mkuu wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Kissa Kasongwa akisikiliza kero za wananchi katika ziara yake aliyoifanya jana Juni 19, 2025 katika kijiji cha Isapulano, Makete. Picha Amiri Kilagalila.

Wakazi wa kijiji hicho akiwemo Sikujua Sanga ameeleza kuwa suala la barabara kwao imekuwa ni changamoto kubwa na kupelekea kushindwa kuyafikia masoko ya mazao, huku watumiaji wengine wa barabara inayopita ndani ya kijiji chao wakilala njiani.

“Inasumbua kwa maana ni mbovu haipitiki hasa kipindi cha kifuku mpaka wanashindwa kusafiri, na wakati mwingine magari yanakwama na kulala baadhi ya maeneo kabla ya kufika kwenye kijiji hicho” amesema Sanga.

Barabara ya Makete-Nkenja inayopita katika kijiji cha Isapulano, ambayo wananchi wanalalamika kutokana na ubovu wake. Picha na Amiri Kilagalila.

Nae Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Makete, Bryson Mwalukisa amesema barabara ya Makete-Nkenja kupitia kijiji hicho yenye urefu wa kilomita 12.5, ilianza kutengenezwa kipande cha kilomita 4.5 kipindi cha masika hali iliyopelekea mkandarasi kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi ambapo kwa sasa wanaendelea na jitihada za matengenezo ya barabara hiyo.

“Lakini pia katika Bajeti ya 2025-2026 ambayo sasa ipo kwenye hatua ya manunuzi, sasa mchakato wa kumpata mkandarasi unafanyika” amefafanua Mwalukisa.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kwa TARURA kuhakikisha wanafanya kazi ya kurekebisha barabara hiyo ili kuondoa adha kwa wananchi, huku pia wakandarasi kwa kushirikiana na TARURA wakitakiwa kurudi kwa wananchi wa kijiji hicho ili kufafanua namna barabara itakavyofanyiwa marekebisho.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW