AU, SADC, EAC zaombwa kuingilia kati sakata la Mwangi, Atuhaire

Na Dominic Allen

Mtandao wa Mshikamano wa Viongozi wa Pan African hii leo umetoa wito kwa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu kuitaka Serikali ya Tanzania kuweka wazi ni wapi alipo mwanaharakati wa Uganda Agather Atuhaire.

Katika taarifa hiyo ya wito uliyowasilishwa na kiongozi wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP) nchini Kenya, Martha Karua, pia umezitaka Kamisheni hizo pamoja na SADC kufanya uchunguzi dhidi ya ya Serikali ya Tanzania kuhusu tuhuma za kushikiliwa na kuteswa kwa mwanaharakati Boniface Mwangi kutoka Kenya pamoja na Agather Atuhaire.

Aidha, Mtandao wa Mshikamano wa Viongozi wa Pan African umesisitiza kutolewa kwa tamko la pamoja la kidiplomasia kulaani kukamatwa kwa wanaharakati hao kinyume cha sheria, ambapo hadi sasa Atuhaire hajulikani alipo.

Mwanaharakati wa Uganda, Agather Atuhaire ambaye alikamatwa nchini Tanzania alipowasili kwa ajili ya kufuatilia kesi zinazomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.

Boniface Mwangi aliachiliwa huru leo, ambapo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, alitelekezwa maeneo ya Ukunda, Kenya baada ya Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora nchini humo kuishinikiza Serikali ya Tanzania kuachiliwa kwake, ambapo alipelekwa jijini Nairobi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mwanaharakati Boniface Mwangi (katikati) katika picha ya pamoja na watu wake wa karibu mara baada ya kuachiliwa huru leo Mei 22, 2025.

Hata hivyo, Agather Atuhaire bado hajulikani wapi alipo licha ya Serikali ya Uganda hii leo kuitaka Serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwake.

Wanaharakati hawa wawili walikamatwa walipowasili nchini Tanzania kwa ajili ya kufuatilia kesi zinazomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Mei 19, 2025.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW