Serikali yaendelea kidhibiti usambaaji wa vimelea vya malaria shuleni

Na Wizara ya Afya

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kudhibiti vimelea vya malaria katika maeneo ya shule za msingi kwa wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la saba, ambao baadhi yao bila kujua wamekuwa wakitembea na vimelea vya malaria na kuwaambukiza wengine au kusambaza katika maeneo ya shule au kurejesha maambukizi majumbani.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria, Dkt. Abdallah Lusasi wakati wa kikao cha mrejesho cha Wadau wa Malaria nchini kilichofanyika jana Mei 23, 2025 mkoani Dodoma.

Dkt. Lusasi amesema katika kutatua hilo serikali imetoa tiba kinga kwa watoto hao wa shule katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tuna tiba kinga kwa watoto wa shule za msingi na tunawapa katika vipindi maalum vya maambukizi wa ugonjwa wa malaria, sasa hivi tunaendelea Nyang’wale na Kibondo, na maeneo yenye maambukizi ya juu,” amesema Dkt. Lusasi.

Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria, Dkt. Abdallah Lusasi (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha mrejesho cha Wadau wa Malaria nchini kilichofanyika jana Mei 23, 2025 mkoani Dodoma.

Pia amesema Serikali imedhamiria kupunguza hali ya maambukizi ya malaria kufikia asilimia 3.5 hadi kufikia mwisho wa mwaka 2025 kwa nchi nzima na kuitokomeza malaria kabisa ifikapo 2030.

“Tuendelee kushirikiana kwa pamoja na wananchi kule chini, asasi za kijamii na kiraia kwakuwa mko karibu na jamii na nyinyi ndio nyenzo wezeshi za kufanikisha hili la kupambana na Malaria na kuitokomeza ifikapo 2030,” amesema Dkt. Lusasi.

Ameongeza kuwa iwapo ushirikiano baina ya Serikali, wadau na jamii utaendelea kuzingatia nguzo za udhibiti wa malaria kwa kila kundi kutimiza wajibu wake na jukumu lake la msingi lengo hilo litafikiwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, wananchi na asasi za kiraia.

Baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao cha mrejesho cha wadau wa Malaria nchini kilichofanyika jana Mei 23, 2025 mkoani Dodoma.

Amegusia pia suala la umuhimu wa matumizi ya takwimu zinvyosaidia kutoa mwelekeo wa mapambano, uelimishaji umma katika kutokomeza malaria sambamba na upatikanaji wa dawa na bidhaa tiba zote za malaria.

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW