Mfahamu mgombea wa Urais nchini Marekani, Chase Oliver

Na Dominic Allen

Chase Oliver, mgombea mwenye umri mdogo zaidi anayewania kiti cha ya Urais wa Marekani kupitia chama cha Libertarian akiwa na umri wa miaka 39.

Maisha yake binafsi

Chase Oliver alizaliwa Agosti 16, 1985 katika jiji la Nashville katika jimbo la Tennessee. Alianza harakati za kulisaka tonge angali na umri wa miaka 13 akifanya kazi kwenye mgahawa.

Mgombea huyu alihitimu elimu yake ya juu katika chuo cha Chuo Kikuu cha Georgia. Katika chuo hiki alipata elimu ya juu na maarifa yaliyomuwezesha kuimarisha uwezo wake wa uongozi na uelewa wa masuala ya kijamii na kiuchumi.

Maisha yake ya Siasa

Oliver aliingia kwenye ulimwengu wa siasa akiwa ni mwanaharakati mnamo mwaka 2010 akipinga vikali vita vya Iraq enzi za uongozi wa Rais mstaafu wa Marekani, George Bush.

Mwaka huo huo aliamua kujiunga na chama cha Libertarian ili kuendeleza harakati zake za siasa.

Mnamo mwaka wa 2020, Chase Oliver kupitia chama Libertarian aligombea nafasi ya katika Baraza la Wawakilishi katika Jimbo la Georgia ambapo alipata kura asilimia 2, lakini hii ilimpatia fursa  ya kuibua mijadala kuhusu uhuru wa mtu binafsi, haki za kiraia, na umuhimu wa mabadiliko ya kisiasa.

Mwaka 2022, alijitosa tena kwenye siasa kwa kugombea nafasi ya Seneta katika Jimbo la Georgia, akichuana na Seneta aliyekuwepo madarakani, Raphael Warnock na mpinzani mwingine, Herschel Walker.

Katika mdahalo uliyowakutanisha Oliver na mpinzani wake Raphael Warnock, Oliver alionekana kuwa mtu huru, akiwakilisha maoni ya wapiga kura waliochoshwa na mfumo wa vyama viwili.

Matokeo ya chaguzi huo wa Seneta katika jimbo la Georgia  hayakuwa mazuri kwa Oliver kwani alipata kura asilimia 2.1, Raphael Warnock asilimia 49.4 huku Herschel Walker akipata asilimia 48.5.

Kwa mara nyingine tena chama cha Libertarian kimempatia ridhaa Chase Oliver kupeperusha bendera ya kuelekea uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba 05 mwaka huu.

Kuelekea uchaguzi huu mgombea huyu anajitahidi kuwavutia wapiga kura waliochoshwa na mvutano wa kisiasa usioisha kati ya vyama vikubwa viwili nchini Marekani ambavyo ni Republican na Democratic.

Akiwa na imani kuwa atafanya vyema katika uchaguzi huu, Oliver ameandaa mipango thabiti ya sera katika kuhakikisha Marekani inafika kule inapotakiwa kufika na amepanga kulifanya Taifa la marekani kuwa na uchumi wenye tija.

Ameahidi akipatiwa ridhaa ya kuwa rais atafunga mianya ya kisheria inayozipa kampuni zenye uhusiano wa karibu na maafisa wa serikali, na ambayo inakandamiza ushindani na ubunifu katika soko huria huku akienda mbali zaidi na kuahidi kuwa atadhibiti matumizi ya fedha serikali.

Kati sekta ya elimu mgombe huyu ametoa ahadi kuwa atalitaka Bunge la Congress kuondoa riba ya mikopo ya sasa kwa wanafunzi.

Chase Oliver anayegombea kupitia chama cha Libertarian anaiona Marekani iliyobora endapo atapatiwa ridhaa ya kuliongoza Taifa hilo.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW