Mfahamu mgombea wa Urais nchini Marekani, Jill Stein

Mfahamu mgombea wa Urais nchini Marekani, Jill Stein

Na Dominic Allen

Jill Stein, ni mgombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi wa Marekani mwaka huu kupita chama cha Green, aliyetangaza nia ya kugombea mnamo November 09, 2023.

Maisha yake binafsi

Jill Stein mwenye umri wa miaka 74 ana asili ya Kiyahudi na Urusi alizaliwa tarehe 14 /05/ 1950 katika jiji la Chicago katika jimbo la Illinois.

Mwanasiasa huyu ameolewa na Richard Rohrer, wakiwa na watoto wa kiume wawili ambao ni Ben Stein (27), na Noah Stein (24).

Alifanikiwa kumaliza elimu yake ya awali huko Highland Park iliyopo Chicago. Mnamo 1973, alihitimu katika Chuo Kikuu cha Harvard akiwa na shahada ya kwanza ya saikolojia, sosholojia, na antropolojia. Mnamo mwaka wa 1979 alihitimu kutoka Harvard Medical School, ambako baadaye alihudumu kama mwalimu wa tiba ya ndani.

Jill Stein ameshafanya kazi ya udaktari katika kliniki za afya huko Boston kwa takriban miaka 25, wakati akifanya kazi ya udaktari, miaka ya 1990, Stein aliona kuna uhusiano kati ya matatizo ya kiafya ya baadhi ya wagonjwa aliyowatibu na athari za kemikali hatari katika mazingira yao..Hivyo alianza kufanya harakati kuhusu mazingira huku akiunga mkono mashirika na taasisi za mazingira nchini Marekani.

Mnamo 2003, Stein alikuwa ni mwanzilishi mwenza wa Massachusetts Coalition for Healthy Communities, shirika lililopigania afya na ustawi wa jamii za Massachusetts, likijumuisha huduma za afya, uchumi wa kijani, ulinzi wa mazingira, haki za wafanyakazi, na demokrasia.

Maisha yake ya Siasa

Katika ulimwengu wa siasa, Jill Stein alionekana kutoridhishwa na Chama cha Democratic huko Massachusetts, hivyo aliamua kujiunga  na Chama cha Green-Rainbow cha jimbo hilo na kugombea nafasi ya ugavana mnamo mwaka 2002.

Stein alishika nafasi ya 3 akipata asilimia 3.4 ya kura, akichwa mbali na wapinzani wake Mitt Romney (asilimia 49.2) wa Republican na Shannon O’Brien wa Democratic aliyepata asilimia 44.4 za kura.

Mwaka 2004, aligombea nafasi katika Baraza la Wawakilishi kutoka jimbo la Massachusetts, alishika nafasi ya pili akiwa na asilimia 21 ya kura.

Licha ya kushindwa kwenye chaguzi hizo, Stein hakukata tamaa, kwani alitupa ndoano yak na kugombea nafasi ya rais wa Marekani 2012 kupitia chama cha Green, ambapo alishika nafasi ya nne, akipata asilimia 0.4 tu ya kura zote.

Stein aligombea tena urais kama mgombea wa Chama Green katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2016, na alishika tena katika nafasi ya nne, lakini safari hii alipata zaidi ya kura milioni 1.4.

Ilikuwa ni mafanikio kwake kwani katika uchaguzi wa urais wa  mwaka 2012 alipata kura 470,000.

Baada ya kushindwa katika chaguzi hizo mbili za Urais, Stein hakugombea nafasi hiyo ya Urais katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Sasa amerejea tena kugombea nafasi hiyo kupitia chama cha Green akiwa na kauli mbiu ya ‘Amani, Sayari, na Watu’.

Kauli mbiu hiyo imebeba mitazamo tofauti ya kisera ya mgombea huyu, na anaamini kuwa Waamerika wanathamini sana suala la uhuru na haki, lakini mamilioni ya watu bado wanapigania haki za kimsingi.

Anasema kuwa endapo ataingia madarakani, atahakikisha uchumi unakuwa sawa kwa wote na siyo tu kwa matajiri nchini Marekani, huku akiahidi kuboresha mazingira ya kazi pamoja vipato kwa wafanyakazi.

Jill Stein anaamini kuwa wahamiaji wanamchango mkubwa sana kwa Marekani kwa ni chanzo za nguvu kazi, hivyo atahakikisha anashughulikia kero wanazokumbana nazo wahamiaji.

Mwanasiasa huyu mwenye ndoto ya kuwa na dunia yenye mazingira bora kwa viumbe vyote, hajaliweka kando suala la mazingira katika kampeni zake na kuahidi kuwa ataweka mipango na mikakati madhubuti ili kutunza mazingira pia ataweka msisitizo katika kuimarisha amani ulimwenguni.

Ikiwa zimebaki siku kadhaa kuelekea kwenye uchaguzi huu, Stein amekosolewa vikali na chama cha Democratic huku wakisema kuwa kumpigia kura Jill Stein ni sawa na kumpigia kura Donald Trump,

Stein anaungwa mkono na Profesa Jeffrey Sachs kutoka Chuo Kikuu cha  Columbia, huku akisema kuwa vyama vikuu vya Democratic na Republican ni vyama vinavyoshindania kuleta vita vikuu vya tatu vya dunia.

Ukosoaji anaokumbana nao Stein haujamwondoa kwenye reli mwanasiasa huyu mkongwe aliyekwepa mishale mingi na anaamini atashinda kwenye uchaguzi huu.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW