Wafamasia waomba kuondolewa kwa kigezo cha mtihani kupata ajira

Na Amiri Kilagalila

Wafamasia Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wameiomba serikali kuondoa kigezo cha mtihani wa Sekretarieti ya Ajira kwa kada hiyo pindi zinapotangazwa nafasi za kazi, badala yake ajira zitolewe kwa vigezo vya chuo wanavyotoka kuliko kufanya mitihani ambayo imekuwa ikiwanyima fursa vijana wenye uwezo wa kazi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wafamasia Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Nzinza hapo jana katika kikao kilichowakutanisha wanachama wa chama hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe, ambapo amesema kuwa hayo ni miongoni mwa maoni yaliyotolewa na wanachama kuelekea mkutano mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika mkoani Arusha.

“Wanachama wamependekeza na kuiomba Sekretarieti ya Ajira kuwa zinapotangazwa ajira basi mfamasia aajiriwe kwa vile vigezo ambavyo chuo kilimwamini badala ya kufanyishwa mtihani, wanasema unakuta mtu amesoma miaka minne na akaenda kwenye mafunzo ya kazi halafu uje kumtathmini kwa mtihani unakuwa umemuonea” amesema Nzinza.

Nzinza ameongeza kuwa wakati wa usahili inaweza kutokea mtu mwenye vigezo na uwezo mkubwa wa kufanya kazi akaweza kusahau kitambulisho sehemu aliyopumzika na kusababisha kukosa nafasi aliyoitarajia kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafamasia Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Nzinza akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wanachama wa chama hicho kujadili masuala muhimu kuhusu kada ya wafamasia. Picha na Amiri Kilagalila.

Aidha, ameeleza kuwa wanachama wa chama hicho wameishauri serikali kuongeza vigezo vya mwanafunzi kusoma kozi ya famasia badala ya kuwa na kigezo cha D mbili kwa kuwa taaluma hiyo kwa sasa imeshushwa thamani.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wafamasia wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini walioshiriki kikao hicho kilichofanyika Mei 12, 2025 katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe. Picha na Amiri Kilagalila.

Nae Kaimu Mfamasia wa mkoa wa Njombe, Sandey Hokololo pamoja na Hilal Masudi ambaye ni mwakilishi wa vyuo kwa upande wa famasia vinavyopatikana Nyanda za Juu Kusini wanasema licha ya marekebisho mengi yanayohitajika katika kada hiyo kwa sasa, lakini pia wanaomba vigezo vya udahili kuongezwa ili kuiheshimisha kada yao.

“Fani yetu inashuka sana kutokana na vigezo vinavyotumika watu kuingia katika famasi, kama mtu unamdahili kwa D mbili hii inashusha sana. Tulikuwa tunaiomba mamlaka iweke vigezo sawa kwa kada zote za afya” ameeleza Hokololo.

Kwa upande wao baadhi ya wafamasia walioshiriki katika kikao hicho akiwemo Bosco Enock kilichowakutanisha na Mwenyekiti wao wa Kanda kwa lengo la kukusanya maoni na kujadiliana mambo mbalimbali juu ya kada hiyo, wameupongeza uongozi kwa kuona umuhimu wa kukutana na wafamasia ili kupata mawazo mbadala yatakayokwenda kukuza kada yao.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW