Mhagama atoa wito kwa Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Mpox

Na Wizara ya Afya

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amewataka Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Mpox kwa kuepuka kukumbatiana na kushikana mikono, kwa kuwa ugonjwa huu unatokana na maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na binadamu ana uwezo wa kumuambukiza mwenzake kupitia majimaji.

Waziri Mhagama amesema hayo leo Machi 15, 2025 kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kinachoongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed ambacho kinahudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wabunge na Wakuu wa Ulinzi na Usalama.

“Tarehe 7 Machi 2025 tulipata taarifa ya uwepo wa tetesi za wahisiwa wenye dalili za vipele na mambo yanayoendana na ugonjwa wa Mpox, ilipofika tarehe 9 Machi 2025 baada ya kukamilisha uchunguzi wa kimaabara tulithibitisha na kutoa taarifa kuwepo kwa wagonjwa wawili wa ugonjwa wa Mpox” amesema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kufatilia kwa kina mwenendo wa ugonjwa huu kwa wale waliotengamana na wagonjwa ili kuvunja mnyororo wa ugonjwa huo na kuhakikisha Watanzania wanakuwa salama na kuumaliza ugonjwa huo kama ilivyokuwa kwa ugonjwa wa Marburg.

“Magonjwa haya ya mlipuko hayana mipaka, ndiyo maana tunakuwa na mifumo ya mitandao kutoka nchi moja kwenda nyingine ili kuwalinda wananchi wake lakini hasa kutoa elimu kwakuwa na utambuzi wa dalili za magonjwa haya na kuchukua hatua za kitaalam zinazoendelea kusisitizwa na wataalam ili kukata minyororo ya kusambaa kwa magonjwa hayo” amesema Waziri Mhagama.

Vilevile, Waziri Mhagama amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanya juhudi katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko na kufanikiwa kuumaliza ugonjwa wa Marburg nchini Tanzania kwa siku 54 baada ya kupita siku 42 bila mgonjwa yeyote wa ugonjwa huo.

“Nchi yetu imetumia siku 54 tu katika kupambana na kuumaliza ugonjwa huu, hii inaonesha ni namna gani Serikali, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejidhatiti katika kusimamia afya za wananchi wake katika kuwekeza kwenye miundombinu, utaalamu na vifaa tiba ili kuhakikisha unapotokea ugonjwa wa mlipuko tunaumaliza kwa haraka na wananchi wananendelea kuwa na afya njema” amesema Waziri Mhagama.

Kwa upekee, Waziri Mhagama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha Sekta ya Afya nchini ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma kwa kuweka vifaa vya uchunguzi ikiwemo Digital X-Ray inayorahisisha huduma za uchunguzi hasa kwa kina mama wajawazito.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha hospitali yetu ya mkoa wa Ruvuma ambayo itakuwa ni kimbilio, na tunataka kuhakikisha pamoja na vifaa vya uchunguzi tulivyoviweka ikiwemo Digital X-Ray, tufike mahala hospitali hii iweze kusaidia katika kutibu na kufanya uchunguzi wa magonjwa makubwa kwa kuweka MRI mashine na nyinginezo” ameeleza Waziri Mhagama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Ahmed Abbas amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha Sekta ya Afya katika mkoa huo pamoja na Wizara ya Afya kwa kupambana na magonjwa ya mlipuko.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW