Mhagama: Bodi za hospitali zitatue changamoto kwa kuzigeuza kuwa fursa

Na Dominic Allen

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amezitaka bodi zote za hospitali hapa nchini kutatua changamoto zilizopo kwa kuzigeuza kuwa fursa kwa kuonesha ubunifu katika usimamizi wa hospitali hizo ili wananchi wapate huduma bora za afya kwa viwango vinavyostahili.

Waziri Mhagama ametoa rai hiyo leo Machi 5, 2025 wakati akizindua Bodi mpya ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Amana jijini Dar es Salaam yenye wajumbe tisa (9) inayoongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. David Sando.

“Siku ya kwanza mnapoanza kazi, changamoto zote zigeuzeni kuwa fursa ili kuwatendea haki wananchi wa Ilala na mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Wizara ya Afya kwa kuwa najua mna uwezo wa kufanya hivyo kwa ubunifu ili wananchi wapate huduma bora za afya” amesema Waziri Mhagama.

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama akihutubia wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Amana jijini Dar es Salaam.

Waziri Mhagama amesema ni matumaini yake kuona bodi hiyo inakuwa kiungo muhimu kwa kufanya mageuzi makubwa katika hospitali hiyo, kwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana matarajio makubwa na bodi hiyo, kwani uhai wa bodi hiyo ni ufanisi katika upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

“Baada ya kuzindua bodi hii leo, utendaji wake utakuwa mzuri, chukueni mazuri ya wenzenu lakini na ninyi pia mje na mazuri mengi ya kwenu kwa kuonesha ubunifu kwakuwa hospitali hii wanakuja watu wengi na wengine kutoka katika Mataifa mengine” ameeleza Waziri Mhagama.

Ili kuhakikisha watumishi wa Hospitali ya Amana wanatekeleza majukumu yao kikamilifu, Waziri Mhagama ameitaka bodi hiyo kukaa na watumishi hao na kusikiliza changamoto zinazowakabili pamoja na kuangalia haki na stahiki zao.

Katika uzinduzi wa bodi hiyo, Waziri Mhagama pia amepokea hundi ya fedha kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 100 kutoka katika Klabu ya Young Africans iliyokabidhiwa na Rais wa Klabu hiyo, Engineer Hersi Said ambazo zitasaidia katika uboreshaji wa miundombinu pamoja na huduma za afya katika hospitali hiyo.

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama akipokea hundi ya fedha kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 100 iliyokabidhiwa na Rais wa Klabu ya Young Africans, Engineer Hersi Said

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW