“Nani alaumiwe?” Wakili Mwabukusi

Na Wakili Boniface Mwabukusi

Katika tafakuri ya kina kuhusu hali ya sasa ya Taifa letu, maswali haya ni ya msingi katika kutafakari chanzo na mzizi wa changamoto tunazokabiliana nazo kama nchi:

Je, lawama zielekezwe kwa washauri wa viongozi wetu ambao wameshindwa kutambua uzito wa majukumu yao kama wasaidizi wa viongozi wa kitaifa katika kulinda Tunu za Taifa — Haki, Utu, Amani, Utulivu na Umoja wa Kitaifa?

Je, ni wasaidizi haohao wa viongozi wetu wanaoendekeza hofu ya kupoteza nafasi zao, kiasi cha kukosa ujasiri wa kutoa ushauri wa haki na hekima? Matokeo yake, viongozi wetu wamejikuta wakigeuzwa kuwa washauri wa washauri?

Je, kuna kupooza kwa mihimili ya dola — hasa Bunge na Mahakama — kiasi kwamba Serikali, kama mhimili mmoja, imejichimbia na kujiona huru kupuuza sheria, kanuni na Katiba kwa kukosekana kwa mfumo wa “checks and balances” katika uwajibishanaji?

Je, ni kushuka kwa maadili na uwajibikaji katika sekta ya umma — jambo linalochochewa na vyombo kama Jeshi la Polisi, Tume ya Maadili, Tume Huru ya Uchaguzi na Tume ya Haki za Binadamu kushindwa kuonekana huru na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu?

Je, tumeshuhudia kifo au kupooza kwa falsafa ya “Undugu na Uzalendo” ndani ya mioyo ya wananchi — hali ambayo imepelekea mgawanyiko mkubwa wa kisiasa, kidini, kikanda na sasa hata kikabila? Na je, hii imetoa nafasi kwa falsafa hatarishi ya “uchawa” — ambapo mtu anajifungamanisha na mtu badala ya kujitolea kwa Taifa?

Je, tunakosa mfumo madhubuti wa kidemokrasia unaoleta usawa katika chaguzi zetu, ili kuhakikisha kuna uwakilishi wa haki unaoendana na idadi ya kura halisi ambazo vyama hupata?

Je, huu mfumo wa sasa wa mshindi kuchukua kila kitu ndio chanzo cha ukosefu wa maridhiano ya kisiasa?

Je, ni watu wema kujawa na hofu ya kukemea maovu na dhuluma, huku watu waovu wakionekana kuwa na ujasiri mkubwa wa kutenda maovu na kuwashambulia watu wema bila woga

Muhimu

Ni lazima Taifa letu lijifunze kufikiri kwa namna mpya — nje ya wigo wa kiburi, ujuaji na ubinafsi.

Taifa letu lipo njia panda. Tulipo sasa si mahali salama, na tunakakoelekezwa si kule tunakopaswa kwenda.

Tunahitaji uongozi wa maono, ujasiri wa kukemea mabaya, na mshikamano wa kitaifa ili kulinusuru Taifa letu kabla halijazama.

(Maoni ya Wakili Boniface Mwabukusi, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika-TLS)

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW