Mfahamu mgombea wa Urais nchini Marekani, Kamala Harris

Na Dominic Allen

November 05, 2024, Taifa la Marekani linaenda kufanya uchaguzi kuamua ni nani atakuwa Rais wa taifa hilo.

Ushindani wa wagombea kutoka vyama vikuu viwili ambavyo ni Republican na Democratic bado ungali mkali, bila kuwasahau wagombea kutoka vyama vingine na binafsi.

Miongoni mwa wagombea hao ni Kamala Harris, mwanasiasa machachari kutoka chama cha Democratic.

Maisha yake binafsi

Kamala Harris mwenye umri wa miaka 59, ni binti wa Donald Harris na Shyamala Gopalan na alizaliwa Oktoba 20, 1964 huko Oakland, California.

Baba yake alikuwa ni Mwanauchumi Profesa katika Chuo Kikuu cha Stanford mwenye asili ya Jamaica. Mama yake Shyamala alikuwa mwanabiolojia na onkolojisti maalumu kwa saratani ya matiti, asili yake ni Tamil Nadu, India.

Akiwa na umri wa miaka 7, wazazi wake walitengana, ilimlazimu kuishi na mama pamoja na dada yake Maya Harris huko Montreal kutoka mwaka 1976 hadi 1981. Wakati huo mama yake alikuwa anafanya kazi katika Hospitali Kuu ya Kiyahudi na kufundisha katika Chuo Kikuu cha McGill7.

Mgombea huyu wa Urais kupitia chama cha Democratic alipata elimu yake ya Sekondari katika Shule ya Westmount, Montreal Canada kuanzia mwaka 1977 hadi 1981.

Safari yake ya elimu iliendelea hadi alipohitimu Shahada ya Uchumi na Sayansi ya Siasa mwaka 1986 katika Chuo Kikuu cha Howard, na mwaka 1989 Harris alipata Shahada ya Uzamili ya Sheria katika Chuo cha Sheria cha California Hastings.

Mnamo mwaka wa 2014, alifunga ndoa na Douglas Emhoff, ambaye ni Wakili, wakiwa na familia kubwa ya mchanganyiko inayojumuisha watoto wao, Ella na Cole Emhoff.

Maisha yake ya Siasa

Kamala Harris ambaye ni mwanachama kindakindaki wa Chama cha Democratic, amewahi kuhudumu kama Mwanasheria Mkuu wa jimbo la California kati ya mwaka 2011 hadi 2017 wakati wa utawala wa Gavana Jerry Brown. Pia alipata nafasi ya kuhudumu kama seneta wa California katika Bunge la Marekani mwaka 2017.

Mwaka 2019 katika kinyanganyiro cha kugombea uteuzi ndani ya chama chake cha Democratic ili kugombea nafasi ya Urais alifanya vizuri katika hatua za mwanzoni, japo mashua yake ya kura ilienda kombo na hivyo kujiengua.

Hata hivyo, Joe Biden Joe akamchagua kuwa mgombea mwenza wake katika nafasi ya Urais kupitia chama cha Democratic mwaka 2020.

Biden alishinda uchaguzi huo, Kamala Harris akakuwa mwanamke wa kwanza na pia mtu wa kwanza mwenye asili ya Afrika na Asia kuwa Makamu wa Rais wa Marekani.

Kama ilivyodesturi kwa Marekani kufanya uchaguzi wa Urais kila baada ya miaka 4, mnamo Julai 21, 2024, Joe Biden alitangaza kuwa hatagombea muhula wa pili. Wakati huohuo, alitangaza kumuunga mkono Kamala Harris katika uchaguzi wa urais wa tarehe 05 Novemba, 2024.

Linaweza kuwa ni jambo rahisi kwa Kamala Harris kupata uteuzi, lakini bado ana changamoto kubwa kumshinda mpinzani wake kutoka chama cha Republican, Donald Trump.

Ndani ya saa 24 tangu Rais Joe Biden kujiondoa kugombea Urais kwa muhula wa pili, kwa mujibu wa timu ya kampeni ya Harris, aliweza kuchangisha zaidi ya Dola za Marekani milioni 81 kwa ajili ya kuendesha kampeni zake.

Hiki kinakuwa kiasi kikubwa zaidi cha pesa kuchangishwa kwa siku moja na mgombea yeyote katika mzunguko wa uchaguzi huu. Hii imempa nguvu ya kifedha Kamala kuendesha kampeni zake pasi na shaka lolote ile.

Kuelekea kwenye Uchaguzi Novemba 05, wachambuzi wa siasa wanaona Harris anaweza kuungwa mkono na wapiga kura weusi.

Mbali na hilo, Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama anamuunga mkono Harris, akiamini ataifikisha Marekani pale inapotakiwa kufika. Pia aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Marekani Dick Cheney anasema kura yake itaenda kwa Harris.

Baadhi ya wanamuziki Marekani kama vile Taylor Swift walionekana kuvutia Kamala Harris na kuahidi kumpatia kura yake.

Kamala Harris alishawahi kuwa mwendesha mashtaka, hii pia inaweza kumwongezea sifa na nafasi ya kushinda uchaguzi, kwani alifanya kazi nzuri ya utekelezaji sheria kabla ya uteuzi wa makamu wa rais 2019.

Kamala Harris amekuwa akipigia kampeni suala la haki ya utoaji mimba, hili miongoni mwa masuala yenye nguvu kwa chama cha Democratic.

Huku upande wa kodi, Harris anasema atatoa faida kubwa za kodi kwa familia huku akiahidi kufidia gharama hizo kwa kuongeza kodi kwa makampuni.

Katika mdahalo wa kwanza Septemba 10, 2024 kati ya Kamala Harris na Donald Trump, Kamala alionekana kumzidi mpinzani wake.

Katika Mdahalo huu, Kamala aliibua masuala mbalimbali kumhusu Donald Trump, ikiwemo suala la ushuru uliyopendekezwa na Trump, huku akiita “Kodi ya mauzo ya Trump”, Trump aliishia kujitetea zaidi dhidi ya mpinzani wake.

Baada ya Mdahalo huo, Trump alisema kuwa hatafanya tena mdahalo na Harris, kwani anahitaji kujikita zaidi kwenye kampeni zake.

Kamala Harris amemchagua Gavana wa Minnesota, Tim Wolzi kuwa Mgombea mwenza. Walz mwenye historia ya kuhudumu kwenye Jeshi la Ulinzi laTaifa marekani kwa muda wa miaka 24 huku akihudumu kwenye Baraza la Wawakilishi kwa miaka 12, sasa anaenda kumsaidia Kamala Harris kusukuma gurudumu hili la ushindi.

Endapo Kamala Harris atashinda nafasi hii ya Urais, anakuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Marekani mwenye asili ya Afrika na India.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW